Mkurugenzi wa masoko wa Vodacom Efraim Mafuru akiongea kwa kusisitiza huku akipigiwa makofi na Hashim Lundenga Na George Rwehumbiza wakati alipokuwa akiielezea nia ya kampuni yake kudhamini Miss Tanzania kwa miaka miwili na kuyaboresha zaidi mashindano hayo ili yaendane na viwango vya kimataifa na kupata wawakilishi watakaoletea sifa Tanzania lakini pia Vodacom yenyewe kwa mara ya kwanza mkataba huo ulisainiwa mbele ya waandishi wa habari na wageni mbalimbali walioalikwa katika uzinduzi huo mithili ya baadhi ya mikataba ya kiserikali ambayo imekuwa ikisainiwa na pande mbili za serikali husika mbele ya waandishi wa habari na mashuhuda mbalimbali, kwa picha zaidi za tukio hilo shuka chini upate kujua kilichojiri jana usiku katika Hoteli ya Regency Park iliyoko Msasani.
Hapa mkataba huo ukisainiwa na pande zote mbili mbele ya mashuhuda kulia ni Hashim Lundenga mkurugenzi kamati ya Miss Tanzania, na George Rwehumbiza Meneja udhamini na Mawasiliano Vodacom ambapo sasa Vodacom itadhamini mashindano hayo kwa miaka miwili na imeongeza zaidi udhamini huo ili kuboresha zaidi mashindano, mwaka jana Vodacom ilidhamini kwa zaidi ya shilingi miloni 600.
Mkurugenzi wa Kamati ya Miss Tanzania Hashim Lundenga kulia na Meneja udhamini na mawasiliano wa Vodacom George Rwehumbiza wakibadilishana mikataba ya udhamini wa shindano hilo mara baada ya kasaini mbele ya waandishi wa habari na wageni mbalimbali walioalikwa katika uzinduzi huo, wanaoshuhudia katikati kuanzia kulia ni katibu mkuu wa kamati ya Miss Tanzania Bosco Majaliwa, Mkurugenzi wa Masoko Vodacom Efraim Mafuru na Miss Tanzania 2008 Nasreem Karim.
Mkrugenzi wa Miss Tanzania Hashim Lundenga akiishukuru kampuni ya Vodacom wakati kamati hiyo na Vodacom walipotiliana saini mkataba wa miaka miwili kadhamini shindano hilo.
Meneja Udhamini na mawasiliano wa Vodacom George Rwehumbiza akizungumzia mafanikio na malengo ya kampuni hiyo katika kuboresha shindano la Miss Tanzania mwaka huu wakati wa uzinduzi wa shindano hilo 2009 na katilana saini mkataba mwingine katika Hoteli ya Regency Park Msasani jana jioni kushoto ni Miss Tanzania Nasreem Karim na mwisho ni Nacte Urio wa Vodacom.
Baadhi ya maofisa waandamizi wa Vodacom kuanzia kulia ni Matina Nkurlu ofisa habari wa Vodacom, Elihuruma Ngowi Meneja huduma za bidhaa Vodacom na Daniel Kijo Brand Executive manager wakiwa katika sherehe za uzinduzi wa miss Tanzania katika hoteli ya Regency Park Msasani jana jioni.
0 comments:
Post a Comment