BONGO5 KUMSAKA MISS KIGAMBONI 2009!!

Mkurugenzi wa Bongo Five Luca Nighest
Kampuni ya Bongo 5 Media Group imeweza kuandaa matamasha mbalimbali hapa nchini ya burudani na kuweza kufanya vizuri na mwaka huu kampuni hiyo imeamua kuandaa Taji la kumtafuta Miss Kigamboni inayotarajia kufanyika mwishoni mwa mwezi wa nne.
Mratibu wa mashindano hayo ambaye ndio mkurugenzi wa Bongo5, Luca anasema ya kwamba mashindano ya mwaka huu ya kumtafuta mrembo wa Kigamboni yatakuwa ya aina yake kwakuwa wameji panga vyema na wanaamini kwamba lazima Miss Tanzania atokee Kigamboni.
“Mwaka huu tumepania kuandika historia ya kwanza kwa Miss Tanzania kwa kutoka katika kitongoji cha Kigamboni, washiriki wanaombwa kujitokeza kwa wingi kwani zawadi za mwaka huu ni nyingi na zenye thamani.” Alisema Luca.
Mbali na hayo alisema form za kushiriki kwenye mashindano hayo zinapatika kwenye ofisi za Bongo5 zilizopo karibu na Posta Mpya mtaa wa Jamhuri na pia zinapatikana online kwa kutembelea HYPERLINK "http://www.bongo5.com/misskigamboni"http://www.bongo5.com/misskigamboni.
Mwisho wa kujaza na kurudisha fomu ni tarehe 5 April hivyo warembo wanaombwa kujitokeza kwa wingi kushiriki kwenye shindano hilo.
Kwa mawasiliano zaidi wasiliana na
+255715009099
+255786712222
+255713946403

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment