Msanii Juma Nature kutoka TMK Wanaume Halisi akishambulia jukwaa wakati wa onyesho lake la uzinduzi wa albam yake Tugawane Umasikini uliofanyika jana kwenye ukumbi w Diamondi Jubilee umati mkubwa wa mashabiki ulifurika kushuhudia onyesho hilo ililofana kutokana na kila msanii kuleta ubunifu wake japokuwa tatizo kubwa lilikuwa ni kuchelewa kwa juma Nature kupanda jukwaani ili kuanza kufanya mambo umasikini uligawiwa kwa watu wengi ila sisi FULLSHANGWE tulifurahia zoezi la kugawa umasikini na burudani iliyokuwepo lakini hatukupokea umasikini huo kwa kuogopa kuwa huenda ndo tukawa masikini moja kwa moja wadau hivyo kauli mbiu yetu tunasema tufanye kazi kwa bidii na kwa kujituma ili tuondokane na huu umasikini, kwa picha mbalimbali za matukio ya onyesho hilo shuka chini mdau upate uhondo zaidi.
Hapa ndiyo palikuwa hapatoshi ilikuwa ni mashambulizi kwa kwenda mbele kama unavyoona katika picha mdau.
Dj Jb kulia ambaye ni mlemavu na Juma Nature wakifanya mambo makubwa jukwaani.
Dj Jb kulia ambaye ni mlemavu na Juma Nature wakifanya mambo makubwa jukwaani.
Mbunge wa viti maalum Al Shaymaa Kwegyir kushoto na Mbunge wa jimbo la Temeke Abas Mtemvu wakibariki zoezi la kuanza kwa mgawo wa umasikini uliofanya na msanii Juma Nature wakati alipozindua Albam yake ya Tugawane Umasikini uliofanyika Diamond Jubilee jana usiku mama Kwegyir alisema ni heri tugawane umasikini huu kuliko wengine wanaokata viungo vya binadamu ili kujipatia utajiri huu ni ukatili na uonevu kwa Albino kati ni watangazaji wa Radio Clouds Adam Mchomvu na Dj Fetty.
Hatimaye naye Ferooz akazindua Policeman yake kwa mbwembwe kibao mapolisi jukwaani mbwa sasa sijui walikuwa wanalinda usalama wake au ndiyo vionjo katika muziki kazi kwenu wadau
Maunda Zorro
Enika Bukuku naye hakuwa nyuma katika shangwe za jana.
Zizzou Fashion kati Mshambuliaji wa Yanga Jerry Tegete kushoto na Juma Pinto wakitafakali kwa pamoja kauli mbiu ya wimbo wa Juma Nature Tugawane Umasikini ilikuwa si mchezo lazima Utafakuri kwa makini ili upate maana ya wimbo huu katika uzinduzi wa Albam hiyo lwenye ukumbi wa Diamond Jubilee usiku wa kuamkia leo.
Mzee wa shamba Afande Sele kama kawaida yake akiwapelekesha mashabiki wake.
Jafarai kushoto nawimbo wake (wali nazi)
Wasanii Q J. kulia na Makamua wakikamua vya kutosha na wimbo wao
Hawa wote waliitikia wito wa Juma Ntaure na wajitokeza kwa wingi ili kugawana huo umasikini na kila mmoja alipata haki yake.
Huyu aliupata vizuri kisha ukamshinda akacheua na kulala fofofo hii ni kali wadau!
Hii ndiyo fulana halali iliyotengenezwa na kundi la TMK Wanaume Halisi kwa ajili ya kuiuza.
Fulana feki zilizotengenezwa na wajaja ili kujipatia fedha isivyo halali zilikamatwa jana katika onyesho laTugawane Umasikini kama anavyoonekana meneja wa TMK Wanaume Halisi King Kiboya Kwaito kulia na mmoja wa wakurugenzi wa Prime Time Godfrey Kusaga wakionyesha fulana hiyo feki kati mwenye kofia ni Juma Nature.
0 comments:
Post a Comment