TUME YA HAKI ZA BINADAMU YALAANI WALIMU KUCHARAZWA VIBOKO!!

Makamu mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora Mahfoudha Alley Hamid akizungumza na wanahabari wakati alipotoa tamko la tume hiyo kulaani kitendo kilichofanywa na mkuu wa Wilaya ya Bukoba cha kuwacharaza viboko walimu wa shule za msingi za Katerero, Kanazi na Kasenene mkoani Kagera kulia ni Bernadeta Gambish Kamisha wa tume hiyo.
TAMKO LA HAKI ZA BINADAMU
Tume ya haki za binadamu na utawala bora imeshtushwa na kusikitishwa sana na taarifa kwamba mkuu wa wilaya ya Bukoba Bwana Albert Mnali, amewachapa viboko walimu wa shuli tatu za Katerero, Kanazi na Kasenene katika mkoa wa Kagera.
Kitendo hicho ni cha ukiukwaji wa haki za binadamu na misingi ya utawala bora kwa mujibu wa sheria za nchi hususan katiba ya jamhuri ya muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 na mikataba ya kimataifa inayolinda haki za binadamuna misingi ya utawala bora ambayo tanzania imeridhia.
Ibara ya 13(6) (e) ya inatamka kama ifuatavyo kuhusu adhabu:"ni marufuku kwa mtu kuteswa, kuadhibiwa kinyama wau kupewa adhabu zinazomtweza au kumdhalilisha."
Tume ya haki za binadamu na utawala bora ambayo ina mamlaka ya kikatiba inalaani vikali kitendo hicho kilichofanywa na mkuu huyo wa wilaya ambaye moja ya majukumu yake ni kulinda haki za binadamu na misingi ya utawala bora.

Uvunjaji wa haki za binadamu na misingi ya utawala bora uliofanywa na mkuu huyo wa wilaya ni pamoja na
- Kutoa adhabu isiyostahili kwani adhabu ya viboko hutolewa na mahakama tu tena kwa kosa la jinailililobainishwa kisheria;

- Kutoa adhabu ya kutweza au kudhalilisha utu ikiwemowalimu wa kike kucharazwa viboko;
-Kuwapa walimu adhabu bila kufuata taratibu za kinidhamu ikiwa ni pamoja na kuwashirikisha maafisa elimu wa Wiliya na Idara ya Utumishi wa Walimu;

Kutumia vibaya madaraka aliyokasimiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na akala kiapo.
Tume ya Haki za Binadamu na utawala Bora inasema kutokana na kitendo hicho cha aina yake na cha aibu hapa nchini kimeleta athari kubwa kwa walimu ikiwemo kuwavunjia heshima walimu kwa wanafunzi wao, familia zao na jamii kwa ujumla pamoja na kuwavunja moyo katika kazi zao za kila siku.
Hata hivyo ingawa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora inalaani kitendi hicho cha Mkuu wa Wilaya, inawataka walimu kuzingatia maadili ya kazi yaoili nao wawatendee haki watoto ya kupata elimu bora badala ya kuwa watoro, wazembe na walevi kama walivyotuhumiwa.
Imetolewa na
Jaji Kiongozi Mstaafu Amir Ramadhani Manento
Mwenyekiti Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment