KOCHA wa timu ya TAIFA ya URUSI, GUUS HIDDINK ameiambia Radio ya taifa ya nchini kwao UHOLANZI kuwa wiki ijayo anatarajiwa kutangazwa kuwa kocha mpya wa klabu ya CHELSEA. HIDDINK mwenye umri wa miaka 62 anatarajia kuchukua jukumu hilo baada ya aliyekuwa kocha wa timu hiyo LUIZ FELIPE SCOLARI kutimuliwa kazi hapo juzi HIDDINK, amesema anachukua jukumu la kufundisha CHELSEA hadi mwisho wa msimu huu baada ya chama cha soka cha URUSI kumruhusu kufundisha timu zote mbili. Kocha huyo ambaye ni raia wa UHOLANZI ni rafiki mkubwa wa mmiliki wa klabu ya CHELSEA, ROMAN ABRAMOVICH na hivi karibuni anatarajia kwenda UINGEREZA kukamilisha kazi ya kwenda kuifundisha CHELSEA.
GUUS HINDDIK AMRITHI SCOLARI CHELSEA!!
Posted by
ADMIN
You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment