AKUDO WAFANYA KWELI USIKU WA SERENGETI OUT OF AFRICA NIGHT (BILLICANAS)!!

Pekechapekechaaaa, Pekechapekechaaa!!!, haya wana wa Akudo Impact vijana wa masauti wakipagawisha usiku wa kuamkia leo kwenye Club ya Billicanas katika usiku wa Serengeti Out of Africa Night kama kawaida Camera ya FULLSHANGWE ilikuwepo kukuletea matukio yote kwa picha ulikuwa ni usiku mzuri na wenye burudani safi iliyotulia wadau kwa matukio zaidi shuka chini uone picha zaidi za tukio hilo.
Dada huyu jamani anaitwa Christabela Mwingira yaani alipata zawadi kwa sababu ya macho yake kufanana na Chui manake yalikuwa yanawaka mithili ya chui si mchezo kama anavyoonekana akikabidhiwa zawadi yake ya bia za Serengeti na Kiongozi wa Akudo Impact Christiane Bella katikati ni Mohamed Bawazir meneja matukio Billicanas.

Huyu ndiye DadaLilian Beberi aliyevalia Kichuichui yaani Serengeti Lager na kujishindia sanduku moja la bia aina ya Serengeti akikabidhiwa zawadi yake na kiongozi wa bendi ya Akudo Impact Christiane Bella kati ni meneja matukio wa Club Billicanas Mahamed Bawazir.

Bahati Singh meneja matukio wa SBL kulia na Mohamed Bawazir meneja matukio wa Club Billicanas walikuwa ni miongoni mwa wawezeshaji wa usiku huo na kuhakikisha watu wanapata raha iliyotarajiwa.

Yaani ilikuwa ni full kushangweka tu kwa raha zao!

Mashabiki waliojitokeza katika usiku huo wa Serengeti Out of Africa Night wakijimwaga stejini.

Twende mbele Turudi nyuma haya mambo hayo wadau!!
Serengeti Out of Africa Night kama kawa yaani ni makamuzi tu kama unavyowaona vijana wa masauti Akudo Impact wakiwakilisha vilivyo kwenye club ya kimataifa Billicanas.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment