Mkurugenzi wa Kampuni ya Benchmarck Production ya jijini ambayo ndiyo inayaendesha shindano la Bongo Star Search (BSS) hapa nchini Maadam Litah Paulsen amezungumza na wanahabari leo katika ukumbi wa idara ya Maelezo juu ya maandalizi na utaratibu utakaotumika kuendesha shindano hilo mwaka huu ambalo litashirikisha mikoa yote ya Tanzania ambayo ni Dar es alaam, Arusha, Tanga, Kigoma, Tabora, Mwanza, Mbeya, Iringa, Mtwara, Dodoma na Zanzibar na amesema shindano hilo linatarajiwa kuanzia katika Jiji la Arusha tarehe 21 February, na washiriki 48 wanatarajiwa kushiriki katika shindano hilo mara baada ya mchujo wa washiriki wa mikoa yote, ameongeza kuwa mtu yeyote anaruhusiwa kushiriki lakini asiwe chini ya miaka 18, ambapo mwaka huu shindano hilo linadhaminiwa na kampuni ya simu za mikononi Vodacom, Litah Paulsen ameongeza kuwa Jaji machachari katika mashindano yaliyopita Salama Jabir pamoja na kuwa kwa sasa yuko nje ya nchi lakini kwenye shindano la mwaka huu pia atakuwepo na anatarajiwa kufanya kazi yake ya ujaji kama ilivyokuwa katika shindano la miaka iliyopita, katika picha aliyeko kushoto ni George Rwehumbiza meneja udhamini na mawasiliano wa kampuni ya Vodacom
BONGO STAR SEARCH 2009 YAJA, SALAMA JABIR KAMA KAWA!!
Posted by
ADMIN
You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment