Mh. Waziri Kapt. George Mkuchika akisisitiza jambo wakati alipoongea na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa wizara hiyo kuzungumzia tamko la serikali kutokana na magazeti ya Taifa Tanzania, Sema Usikike na Taifa leo kuandika na kuchapisha habari zinazodaiwa kuwa za kuchafuana, wamiliki na wahariri wa magazeti hayo wamepewa siku 7 kuanzia leo kuandika maelezo na kuyapeleka kwa msajiri wa magazeti Idara ya Habari Maelezo.
Mh Waziri Kapt. George Mkuchika akionyesha gazeti la sema usikike wakati alipoongea na waandishi wa habari katika ukumbi wa mikutano wa Wizara hiyo leo Serikali imetoa siku 7 kuanzia leo kwa wamiliki wa magaezrti hayo kujieleza kwanini wasichukuliwe hatua za kinidhamu kutokana na kuandika habari za kuchafuana.
Serikali ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania kupitia kwa waziri mwenye dhamana ya Habari Utamaduni na Michezo Kapt. George Mkuchika imetoa tamko kali kufuatia mwenendo wa baadhi ya vyombo vya habari hususan magazeti hapa nchini kutokana na kuandika habari za kukashifiana ambazo zimekuwa zikijichomoza katika baadhi ya magazeti siku za hivi karibuni.
Akizungumza na waandishi wa habari katika wizara hiyo waziri Mkuchika ameyataja baadhi ya magazeti yaliyochapisha habari mbalimbali za kuchafuana kwa baadhi ya wamiliki wa vyombo hivyo, magazeti hayo ni Taifa Tanzania toleo No 052 la Tarehe 6-12 februari 2009 lililochapisha habari iliyosomeka (Harusi ya Mengi sasa yazua utata) gazeti la Taifa letu toleo No 00487 la february 9. 2009 lenyewe lilikuwa na habari isemayo (Karamagi adaiwa kudandia wake za vigogo wenzake, Avunja ndoa ya Mkuu wa Wilaya) na gazeti la Sema Usikike Toleo No 002 la tarehe 10 februari 2009 lenyewe liliandikwa ("Waziri Mkuu wa Zamani amweka kimada Shoga... Shoga mwenyewe ni Mwanasiasa mwenzake..").
Waziri Mkuchika ametoa siku saba kuanzia leo tarehe 7-19 mwezi huu kuwa wamiliki wa magazeti hayo na wahariri wake kuandika maelezo na kuyawasilisha kwa msajiri wa magazeti katika Idara ya habari maelezo kwamba kwanini wasichukuliwe hatua za kinidhamu kwa kitendo hicho cha kuandika habari za kuchafuana kutokana na sheria ya magazeti ya mwaka 1976.
Amesema kuwa kwa kuwa sasa sheria ya magazeti ya mwaka 1976 ndiyo inafanya kazi na sheria mpya bado haijakamilika hatuwezi kuenda bila sheria yoyote na tukaacha watu wanafanya mambo wanavyotaka, hivyo kwa kutumia sheria hii hii ya mwaka 1976 nitawashughulikia watakaokiuka maadili ya uandishi wa habari kwani sheria hii inanipa mamlaka ya kuwashughulikia wanaofanya kinyume na utaratibu na maadili ya kupasha habari.
0 comments:
Post a Comment