JAJI MKUU AGUSTINO RAMADHANI AMEWAAPISHA MAOFISA MBALIMBALI WA MAHAKAMA LEO!!


Jaji mkuu wa Tanzania Agustino Ramadhan akimwapisha Bw. John Mgeta kuwa Kaimu Naibu Msajili wa Mahakama Rufani Tanzania leo katika ukumbi wa mahakama ya rufaa Tanzania jijini Dar es salaam.Upande wa kulia wa jaji mkuu ni Kaimu jaji kiongozi kanda ya Dar es salaam Aristoclas Kaijage.


Jaji mkuu wa Tanzania Agustino Ramadhan akipeana mkono na Bi. Happines Ndesamburo mara baada ya kuapishwa kuwa Kaimu Naibu Msajili wa Kitengo cha Biashara Mahakama kuu kanda ya Arusha katika sherehe fupi iliyofanyika leo katika ukumbi wa Mahakama ya Rufaa jijini Dar es salaam.

Jaji Mkuu wa Tanzania Mh. Agustino Ramadhan(mstari wa mbele katikati) katika picha ya pamoja na maofisa wa mahakama (waliosimama mstari wa nyuma) mara baada ya sherehe fupi ya kuwaapisha kushika nyadhifa mbalimbali leo jijini Dar es salaam.





You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment