Kweli mtoto wa kike ni kivazi manake maneno haya niliwahi kuyasikia siku moja pale maisha Pub nilipokwenda kujipatia shangwe zangu usiku mmoja nikasikia akina dada kadhaa wakisema "mwanamke kivazi bwana" lakini siku nyingine nilipokwenda kwenye onyesho la wanamuziki wanne wakubwa kutoka Marekani na Nigeria yaani Fat Joe, Eve na P. Square lililofanyika pale Gymkana mwishoni mwa mwaka jana kulikuwa na vimwana wengi wakiwa wamejipigilia vivazi vilivyovutia wengi majawapo ni hiki aalichokuwa amevaa mnenguaji wa Bendi ya Afrcan Stars Twanga Pepeta Lilian Enternet anayeonekana katikati katika picha wakati alipopanda jukwaani kushangweka pamoja na mwanamuziki Eve alipokuwa akitumbuiza
Haya msimu wa mashindano ya Miss Tanzania kwa mwaka huu 2009 ndiyo huo unakaribia sijui Mkurugenzi wa Miss Tanzania Hashim Lundenga kama anavyoonekana kushoto na waandaaji wa mikoa na kanda watakuwa wamejiandaaje mwaka huu ili kuyafanya mashindano hayo yaweze kuboreshwa zaidi najua ni kazi ngumu kuwaridhisha watu lakini kamati hiyo haina budi kuhakikisha inaboresha zaidi ili shindano hilo liweze warembo wenye viwango zaidi na kuvutia watazamaji wengi hapa nchini na kwingineko huyo kulia ni mwandaaji wa Miss Ilala Jackson Kalikumtima.
Kumekuwepo na tatizo la utupaji hovyo wa takataka mijini kitu ambacho kimepelekea watoto wengi kujitafutia vitu mbalimbali katika taka hizo na kuviuza kama sio kuvitumia wao wenyewe hii imekuwa na athari kwa afya zao kutokana na mazingira yenyewe kuwa machafu kwa kiwango cha hali ya juu FULLSHANGWE tunawaomba wahusika waache mara moja kutupa taka hovyo kwani zinahatarisha maisha ya watoto ambao wengi wao hawajui kuwa maeneo hayo ni hatari kwa afya zao kama wanavyoonekana watoto hawa wakiokota takataka katika moja ya mitaa ya jiji .
0 comments:
Post a Comment