EVE E ASHANGILIA OBAMA! OBAMA!, LAKINI PIA ASEMA NAWAPENDA SANA MBWA WANGU!!

Eve E akionyesha michoro ya Tatuu katika mwili wake wakati alipoongea na waandishi wa habari jana kwenye Hoteli ya Kilimanjaro Kempiski.

Mwanamuziki Eve E kutoka Marekani ambaye alikuwa hapa nchini kwa onyesho moja lililofanyika jana kwenye viwanja vya Gymkana amesema katika vitu ambavyo anavipenda katika maisha yake ni pamoja na mbwa wake watatu ambao anawafuga huko nyumbani kwake.

Eve E ameyasema hayo katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika kwenye hoteli ya Kilimanjaro Kempiski kabla ya kupanda jukwaani jana, mwanamuziki huyo ameeleza hayo wakati akijibu moja ya swali aliloulizwa na mwandishi mmoja aliyeomba kutajiwatajiwa majina ya mbwa wake watatu ambao mwanamuziki huyo alidai anawapenda sana wakati akifanya mahojiano na moja ya kituo cha redio Clouds hivi karibuni kabla hajawasili nchini.

Eve E ambaye amekiri kuwa nao hao mbwa na amesema ni kweli anawapenda sana mbwa wake, katika mahojiano na kituo cha Radio Clouds cha jijini, Eve alisema "huko kwetu marekani tunayo siku moja inayoitwa (Thanks Giving) ambayo wamarekani wengi hupenda kusherekea siku hii wakiwa na Familia zao nyumbani lakini mimi nimekuwa nikisherekea siku hii nikiwa na mbwa wangu wazuri nyumbani kwangu ambao majina yao ni Spanks, Bear na Monkey"

Eve E Alipoulizwa kuwa anajisikiaje Barrack Obama kuchaguliwa kuwa Rais mpya wa Marekani kutoka Chama cha Democratic Eve ameshangilia akinyoosha mkono juu na kusema "Obama! Obama! Obama!", ikiwa ni ishara kuwa anamkubali sana Rais huyo mteule wa Marekani.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment