ULUGURU MOUNTAIN GOLDEN FACE KHANGA FASHION YAJA!


Mratibu Alex Nikitas


Maonyesho ya mavazi yaliyopewa jina la Uluguru Mountain Golden Face Khanga Fashion yanatarajiwa kufanyika mkoani Morogoro Tarehe 17-31/10/2008 katika ukumbi wa Vijana Social hall na Hotel Oasis mjini humo.



Akizungumza na Fullshangwe mratibu wa maonyesho hayo Bw. Alex Nikitas amesema wabunifu wengi kutoka mkoani Morogoro watashiriki katika maonyesho hayo ili kuonyesha vipaji vyao katika ubunifu wa mavazi.



Amewataja wabunifu watakaoshiriki katika maonyesho hayo kuwa ni Nasero Fashion, Rukia Ndege Fashion, Dulla Fashion Fine Faborouse Boutiqe na wengine wengi ambapo mbunifu Masoud Kipanya Maarufu kama KP yeye ni mbunifu mwaalikwa atakayetoka Dar es alaam.



Maonyesho hayo yamedhamini wa na kampuni ya simu za mikononi TIGO na burudani italetwa na msanii wa kimataifa mtanzania kutoka Afrika kusini anayeitwa Kibuti aka (Kiboot) wapenzi wote wa Burudani ya Mitindo mnakaribishwa amemaliza Alex Nikitas.




You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment