Mgeni Rasmi Waziri wa Kazi, Ajira na Maendeleo ya Vijana Prof. Athman Jma Kapuya akiongea na vijana wakati wa kongamano la vijana lililoandaliwa na Asasi ya Vijana ya Umoja wa Mataifa YUNA na kufanyika ukumbi wa APEADU kwenye ofisi za Umoja huo mtaa wa Mafinga Kinondoni Jijini Dar es salaam katika kuadhimisha siku ya vijana Duniani.
Katika kongamano hilo vijana wamejadili mambo mbalimbali yanayowahusu kama vile Elimu, Afya, Ajira, Michezo, Haki zao na mambo mengine mengi wanayokumbana nayo katika maisha ya kawaida kama vijana huku wakiazimia kuomba Serikali iwaruhusu kuunda Baraza la Vijana la Taifa litakalosimamia mambo yao yote ili kuwatetea na kuwasimamia katika mipango mbalimbali ya Kisera inayowahusu vijana.
Katika Hotuba yake Waziri Kapuya amewaasa vijana kuunda Baraza litakalokuwa ni la kitaifa zaidi kuliko kuwa Baraza la kiubabaishaji linaloweza kuleta athari kubwa kwa taifa Waziri pia alizindua mwaka wa Vijana unaoanza leo tarehe 12 Agosti 2010 mpaka Agosti 11 , 2011 na utakuwa ukiadhimisha kila mwaka Duniani kote.
Waziri wa Kazi, Ajira na Maendeleo ya Vijana Prof. Athman Juma Kapuya akiingia kwenye ukumbi wa mkutano wa kati wa kongamano la vijana lilioandaliwa na Asasi ya Vijana ya Umoja wa Mataifa YUNA na kufanyika ukumbi wa APEADU kwenye ofisi za umoja huo Mtaa wa Mafinga Kinondoni jijini Dar es salaam nyuma ya Waziri ni Mwakilishi wa UNIDO Nchini Emmanuel Kalenzi.