Karibu watu 700 wakiwemo watoto wametekwa kwa nguvu kutoka nyumbani kwao kwenye maeneo ya vijijini katika Jamhuri ya Afrika ya kati na kaskazini mwa Jamhuri ya demokrasi ya Congo.
Asili ya kundi la Lord's Resistance Army,linaloongozwa na Joseph kony,ni Kaskazini mwa Uganda.Leo hii wapiganaji wake wako hadi Congo kaskazini,Sudan Kusini na mashariki mwa Jamhuri ya Afrika ya Kati.
Shirika la kutetea haki za binaadamu la Human Rights Watch linasema kuna ushahidi kwamba kundi hilo limekuwa likiteka watu nyara kufwatia amri ya Joseph Kony.
Habari kwa hisani ya www.bbcswahili.com
0 comments:
Post a Comment