Kaberuka achaguliwa tena kuwa Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB)


Bodi ya Magavana wa Benki ya Maendeleo ya Afrika leo tarehe 27 mwezi mei hapa Abidjan imemchagua tena Bw.Donald Kaberuka kuwa Rais wa Benki hiyo kwa kipindi cha pili. Bw. Kaberuka alichaguliwa kwa mara ya kwanza kuwa Rais wa Benki hiyo mwaka 2005.

Kuchaguliwa kwake kwa kipindi cha pili kumetokana na mafanikio makubwa ambayo ameyaleta katika benki hiyo na kuleta maendeleo katika taasisi hiyo muhimu ya kifedha na kwa bara la Afrika. Hii ilibainika kutoka kwa Magavana waliotaka Rais huyo kuendelea na wadhifa wake.

Katika kukubali kuthibitishwa kwake katika cheo hicho. Bw Kaberuka aliwashukuru Magavana hao kwa kuwa na imani na uongozi wake katika benki. “Nina farijika sana kuona kuwa ninyi Magavana mna imani kubwa na mimi hadi kunichagua tena ili niweze kuiongoza taasisi hii muhimu, kwa kweli nina shukuru sana”,alisema.

" Ningependa kutoa shukrani zangu za pekee kwa uongozi na wafanyakazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika kwani wao ndio wamenifikisha hapa kwani mimi ni Rubani tu. Alisema Kaberuka baada ya kuthibitishwa katika nafasi hiyo.

“Nilichaguliwa kwa mara ya kwanza miaka mitano iliyopita.Benki imeongezeka mara mbili . Lakini katika kipindi cha miaka mitano ijayo, tutajikusanya na kuiweka Afrika katika kiwango cha juu kimataifa",alieleza.

"Tutajitahidi kuhakikisha kuwa tunafikia mategemeo ya watu wa Afrika. Tutafanya kazi ilitufikie lile lengo la kuwa na bara moja linaloshirikiana kwa kila kitu, tutapambana na mabadiliko ya hali ya hewa na kuhakikisha kuwa tunakuwa na chakula cha kutosha, alisema.

Kikosi cha Benki ya Maendeleo ya Afrika kimekuwa na maendeleo makubwa katika shughuli zake za ndani na uongozi, vilevile imelenga zaidi uwajibikaji katika kuleta maendeleo Afrika hasa katika kukuza sekta binafsi, kufadhili miradi inayoshughulikia miundo mbinu, na kusisitiza kuwepo biashara ya pamoja katika kukuza uchumi wa bara la Afrika.

Katika ripoti iliyotoka hivi karibuni inayohusu muonekano wa Uchumi katika Bara la Afrika inasema kuwa, ifikapo mwaka 2011 uchumi utakuwa kwa asilimia 5.2 tofauti na kiwango cha sasa cha asilimia 4.5 kwa mwaka 2010.

Kwa sababu ya kuongezeka kwa mahitaji ya Benki ya maendeleo ya Afrika Benki imekuwa na uhaba wa fedha uliosababishwa na mtikisiko wa uchumi. Kwa sababu hiyo basi Magavana pia wametoa uhalalisho wa kuongeza mtaji kwa taasisi zake kwa asilimia 200% hii itasaidia kuendesha miradi na programu ambazo nchi wanachama imezipanga.

Chini ya uongozi wa Bw. Kaberuka Benki imejitahidi kuhakikisha kuwa kunakuwa na mawasiliano ya karibu kati ya nchi zilizoko kwenye ukanda mmoja na sekta binafsi. Aidha benki imefanikiwa kuwa na ofisi katika kila nchi barani Afrika.Magavana waliainisha.
Bw. Kaberuka, ambaye ni Rais wa saba wa Benki ya Maendeleo ya Afrika, aliapishwa tarehe 1 mwezi septemba mwaka 2005 kwa mara ya kwanza huko Tunisia.

Kabla ya kujiunga na Benki, Bw. Kaberuka alikuwa Waziri wa fedha na mipango ya Uchumi wa Rwanda kuanzia mwaka 1997 mpaka 2005, na alitambulika kama Mkuu aliyejenga upya nchi ya Randa ambayo ilikuwa na vita na aliweza kuijenga nchi hiyo kwa kuweka programu nzuri zilizoleta mabadiliko ya uchumi.

Alianzisha na kuendeleza maboresho katika uongozi na uchumi mkuu katika mambo ya fedha, mambo ya mabenki, bajeti, miundo muhimu ya nchi ikiwa ni pamoja na benki kuu ya nchi iliyo huru. Na matokeo ya maboresho hayo ni kukua kwa uchumi wa Rwanda ulio imara na kuiwezesha nchi hiyo kufaidika kwa kufutiwa madeni yake mwezi Aprili mwaka 2005.

Bw. Kaberuka anauzoefu wa zaidi ya miaka 12 katika mambo ya Benki, katika mambo ya fedha na biashara, katika mambo ya biashara ya vitu kimataifa na katika maendeleo ya sekta kabla yakujiunga na serikali.

Akiwa Waziri wa Fedha na mipango kiuchumi, Rais huyu wa Benki ya maendeleo ya Afrika alitumika kama Gavana wa Benki ya Dunia kwa Rwanda, vilevile katika shirika la fedha la kimataifa na Benki ya Maendeleo ya Afrika.

Alisoma Tanzania hadi kidato cha sita na kupata shahada ya kwanza katika chuo kikuu cha Dar es salaam. Vilevile alisoma Uingereza ambapo alipata shahada ya uzamili katika filosofia ya Uchumi na uzamifu katika filosofia ya Uchumi huko chuo kikuu cha Glasgow - Scotland.
Bw. Kaberuka anazungumza vizuri sana Kiingereza, Kifaransa na Kiswahili.
Ingiahedi Mduma
Msemaji Mkuu- Wizara ya fedha na Uchumi
Abidjan

ALI CHOKI AJA NA MPYA YA IGWEEE MSASANI CLUB!!

Ali Choki aliingia na staili ya aina yake ndani ya ukumbi wa Msasani Club jana usiku tayari kwa utambulisho wa Bendi yake ya Extra Bongo. Baadae staili hiyo ilikuja kujulikana kama Igwee...! Choki haishi Vituko, Ni Burudni yaani kushangweka tu kila mtu kwa raha zake!
(Picha zote kwa hasani ya blogu ya www.mjengwa.blogspot.com )
Ali Choki akiongoza kikosi kizima cha Extra Bongo wana wa kujinafasi, watoto wa mjini katika kulisakata Sebene lao jipya wakati wa kutambulisha bendi hiyo kwa mashabiki waliohudhuria katika onesho hilo..

Hawa sio Wacheza Shoo, ni wanachama wa Extra Bongo wana wa Kujinafasi, na hivi ndivyo walivyoshaini jana usiku ndani ya Msasani Club.

OSCAR SHELUKINDO NA MZEE MKOLWE SAFARINI FRANKFURT!!

Meneja wa kilaji cha Ndovu Oscar Shelukindo na Mpishi Mkuu wa TBL Mzee Gaudence Mkolwe wakiondoka Dar es salaam leo kuelekea Frankfurt, Ujerumani, kupokea tuzo ya Dhahabu ambayo Ndovu imepata kwa kuwa kilaji bora duniani.

HAWA NDIYO VIMWANA WA MISS DAR CITY CENTRE!!

Hapa wakiwa kambini kwenye Hoteli ya Lamada jijini Dar es salaam siku ya ijumaa mara baada ya kuzindua rasmi kambi ya warembo hao picha kwa hisani ya
www.burudan.blogspot.com .
Mwanahabari Super D Mhamila kulia akishoo love na warembo wa Miss Dar City Centrejuzi

MAKAMU WA RAIS AZINDUA MBIO ZA MWENGE WA UHURU!!


NA JOSEPH ISHENGOMA-MAELEZO, Manyara

Makamu wa Rais Dr. Ali Mohamed Shein leo amezindua mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka huu (2010) katika sherehe zilizofanyika katika uwanja wa Kwaraa mjini Babati Mkoani Manyara.Ujumbe wa mbio za Mwenge mwaka huu umezingatia maeneo makuu mawili.

Eneo la kwanza ni mapambano dhidi ya ugonjwa wa malaria na UKIMWI chini ya kaulimbiu, “Maliza Malaria” na “Malaria haikubaliki.” “Zuia UKIMWI Timiza ahadi yako.” “Huduma za UKIMWI ni Haki za Binadamu kwa wote.” Na sehemu ya pili ay ujumbe wa mbio za Mwenge wa uhuru ni uchaguzi Mkuu mwaka 2010 chini ya Kaulimbiu, “Kumbuka hatima ya leo na kesho ya Watanzania imo mikononi mwako, jitokeze kupiga kura.”

Akihutubia wakati wa uzinduzi huo baada ya kusimikwa rasmi kuwa mzee wa Manyara, Makamu wa Rais amewataka wananchi kushiriki kikamilifu katika uchaguzi mkuu ujao na kuwakataa wagombea wote watakao hamasisha vitendo vitakavyoashiria uvunjufu wa amani na utulivu wa Taifa.“Wale wote ambao watajihusisha na kuhamasisha chuki, utengano na ubinafsi miongoni mwa jamii, wakataeni kwani hawafai kuwa viongozi na watakuwa wamepungukiwa sifa za uongozi,’ amesema. “Kila mmoja ahakikishe anatumia haki yake ya msingi kushiriki katika ucahaguzi na kuzingatia sheria mpya ya fedha za uchaguzi na kujiepusha na mambo yote yaliyokatazwa katika sheria hiyo.

Kuhusu mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi, amekemea na kuwalaani watu wanaofanya mauaji hayo ambao amesema kuwa wana roho za kikatili na kutokuwa na imani na ubinadamu kwa ndugu zetu albino.“Wananchi mnaombwa kutoa ushirikiano wenu kwa kuwafichua wale wote wanaojihusisha na ukatili huu.

Serikali kwa upande wake itahakikisha vitendo vya ukatili na mauaji dhidi ya watu wenye ulemavu wa ngozi vinakomeshwa mara moja,”Mauajii ya watu wenye ulemavu wa ngozi yalianza nchini mwaka 2006 katika mikoa ya Shinyanga na Tabola na sasa yamekwisha samba nchi nzima ambapo jumla ya watu 40 wamekwisha uawa na wengine wanane wamejeruhiwa vibaya.

Aidha kuhusu ugonjwa wa Malaria, amesema ugonjwa huo unaoongoza kwa maudhurio ya wawagonjwa wanaofika kwenye vituo vya kutolea huduma ya afya ambao ni kati ya asilimia 30 hadi 40 umekuwa mzigo mkubwa unaoelemea utoaji wa huduma za afya nchini.”Maudhurio hayo ni sawa na asilimia 30 hadi 40 ya maradhi mengine.

Kwa wastani ugonjwa huu wenye kinga umuua mtu mmoja kila dakika tano wengii wao wakiwa watoto wenye umri chini ya miaka mitano na Mama wanajwazito” amesema na kuongeza kuwa lengo la serikali ni kupunguza idadi hiyo ya vifo kwa asilimia 50 ifikapo 2013.Kuhusu madawa ya kulevya, Makamu wa Rais amewaagiza viongozi wa mikoa, manispaa, halmashauri za wilaya na taasisi mbalimbali kuhakikisha anakuwa na mipango endelevu ya ushirikishwaji na ushiriki wa wananchi wote katika kupambana na tatizo la madawa ya kulevya.“Matumizi ya daw za kulevya usababisha ukosefu wa huduma muhimu katika familia.

Na watumiaji wake hukosa busara za kutosha kufanya maamuzi juu ya namna ya kuilinda afya yake. Ili kuepuka tatizo hili., viongozi wa ngazi mbalimbali kuaanzia ngazi ya Taifa, mkoa, halmashauri na mashirika mbalimbali, lazima kuweka mipango mikakati na kuwashirikisha jamii katika mapambano haya.”Baada ya Makamu wa Rais kuzindua mbio hizo zilizoudhuriwa na viongozi mbalimbali akiwemo Waziri wa Kazi, Ajir ana Maendeleo ya Vijana Prof.

Juma Kapuya na WAziri wa Kazi, Vijana Maendeleo ya Wanawake na watoto Zanzibar Mhe. Asha Abdallah Juma, waakilishi wa mikoa ya Kagera, Kigoma, Mwanza, TAbora, Singida, Arusha, Kilimanjaro, Tabora Mara, Pwani na Shinyanga, Mwenge huo umekabishiwa kwa Mkuu wa mkoa wa Manyara Bw. Henry Shekifu ambaye pia amaukabidhi kwa uongozi wa wilaya ya Babati ambayo imekuwa ya kwanza mwaka hu kuukimbiza.

Mwenge huo unatarajiwa kumaliza mbio zake mkoani Manyara tarehe 2/6/2010 na kuendelea na mbio zake mkoani Arusha.

Kitaifa kilele cha mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka huu kinatarajiwa kuwa mkoani Kigoma Oktoba 14, 2010.

CONSOLATA LUCA ANYAKUA TAJI LA MISS TABATA 2010!!

Miss Tabata 2010 Consolata Lucas akipungia mkono mashabiki mra baada ya kutangazwa mshindi katika shindano lililofanyika usiku wa kuamkia leo kwenye ukumbi wa Dar West Tabata jijini Dar es salaam usiku wa kuamkia leo kulia ni mshindi wa tatu Lilian Andrew na kushoto ni mshindi wa pili Sinthia Bavu.
Washiriki waliofanikiwa kigia tano bora ya Miss Tabata 2010 kuanzia kulia ni Sinthia Bavu, Harrieth Mulumba, Doreen Deus, Lilian Andrew na Consolata Lucas.
Vazi la Ufukweni.
Wanenguaji wa bendi ya African Stars wakifanya vitu vyao jukwaani wakati wa shindano la Miss Tabata lililofanyika jana kwenye ukumbi wa Dar West jijini Dar es salaam.
Baadhi ya Majaji wa Miss Tabata kulia ni Ayoub Ryoba na kushoto ni dada Neema kutoka Lady Choice Saloon wakiteta mambo kadhaa juu shindano hilo lililofanyika jana kwenye ukumbi wa Dar West Tabata.
Washika dau wanapoteta utawaona tu kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Kamati ya Miss Tanzania Hashim Lundenga, mandaaji wa Miss Chang'ombe Tom Chilala ambaye shindano lake linafanyika juni 4 pale TCC Chang'ombe na mwisho ni Benny Kisaka Mkurugenzi wa BMP inayoandaa Miss Temeke wanaonekana wana mazungumza mazito juu msimu huu waurembo.
Dominic Nyalifa wa Chanel 5 akichukua mawasiliano kwa wanamuziki wa Twanga Pepeta bila shaka anataka kuandaa bonge la kipindi kwa ajili ya burudani.
Kwa staili hii lazima picha bomba ipatikana si mnaona wenyewe wadau mambo ya Chanel 5 hayo.

Jamaa akataka kuleta rapsha akawahiwa kama unavyowaona mabaunsa wakimyanyua juujuu na kutolewa nje.

Mourinho sasa ni meneja wa Real Madrid!!


Klabu ya Real Madrid ya Uhispania imetangaza kwamba itamjulisha Jose Mourinho rasmi kwa mashabiki wao, Jumatatu ijayo.

Mourinho atajulishwa kwa mashabiki wa Real siku ya Jumatatu
Klabu kilitoa taarifa kuthibitisha hayo.

Marais wa vilabu vya Inter Milan ya Italia, na Real Madrid, walikutana Ijumaa mjini Milan, Italia, kutatua masuala yote, hasa ya kifedha, kuhusiana na Jose Mourinho kuhama kutoka Inter, na kuelekea Uhispania.

Real Madrid wameshawahi kunyakua ubingwa wa Ulaya mara tisa.
Jose Mourinho anaondoka Inter baada ya msimu uliokuwa wa fanaka mno, kupata ushindi katika mashindano matatu muhimu Italia, ikiwa ni pamoja na kuwa klabu bingwa barani Ulaya.
Hata hivyo klabu ya Inter haikutoa maelezo kamili katika taarifa hiyo, kuhusu mapatano hayo kati ya rais wa klabu Massimo Moratti na mwenzake wa Real, Florentino Perez.

Lakini vyombo vya habari nchini Uhispania vimekuwa vikielezea kwamba Inter watapata euro milioni nane, ambazo ni sawa na dola milioni 9.80.

Mourinho aliiongoza Inter kupata vikombe vitatu muhimu, na alimalizia kwa ushindi katika fainali ya klabu bingwa Ulaya, dhidi ya Bayern Munich ya Ujerumani katika uwanja wa Bernabeu, mjini Madrid.

HII ITAKUWA NDIYO KUMBUKUMBU YA BARABARA YA TANGA-HOROHORO!!

Rais Jakaya Kikwete pamoja na Rais wa Mfuko wa Changamoto za Milenia (MCC) kutoka Marekani Daniel Yohannes leo wakimwagilia maji katika mti wa kumbukumbu uliopandwa jana wakati wa uwekaji wa jiwe la msingi katika Ujenzi wa Barabara ya kutoka Tanga hadi Horohoro yenye urefu wa km65 ambayo itagharimu shilingi bilioni 78.05 na ujenzi unafanywa na kampuni ya Sinohydro corporation Limited kutoka China
(Picha na Mwanakombo Jumaa-MAELEZO)

MAKAMU WA RIAS DR. MOHAMED SHEIN KATIKA ZIARA MKOA WA MANYARA!!

Inamuonyesha Makamu wa Rais Dr. Mohamed Shein akivishwa Skafu na Elizabeth Gasper wa Shule ya Sekondari ya Babati Day ,alipotembelea Mkoa wa Manyara akisubiri kuzindua mbio za Mwenge zinazotegea kuzinduliwa mjini Babati leo tarehe 29.5.2010.
Makamu wa Rais Dr. Mohamed Shein wa pili (kulia ) akitoka nje ya ukumbi baada ya kupokea taarifa ya Wilaya ya Babati na anaemfuata wa (pili kushoto) ni Mkuu wa Mkoa wa Manyara ndugu Hendry Dafu Shekifu na wa kwanza kushoto ni Waziri wa kazi Maendeleoya vijana Zanzibar Mhe. Asha Abdallah Juma wakimsindikiza mgeni huyo mjini Babati jana.

Ni Makamu wa Rais Dr. Mohamed Shein (wa tatu kulia akisikiliza Risala ya Wilaya ya Babati kwa kiongozi aliyeteuliwa ambae hayupo pichani na wengine wa kwanza kulia ni Waziri wa kazi Maendeleo ya Vijana Zanzibar Mhe. Asha Abdallah Juma anaefuata ni Waziri wa kazi na Maendeleo ya Vijana Tanzania bara Mhe. Juma Kapuya na wa pili kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Manyara ndugu Hendry Shekifu akifurahia Risala hiyo jana kwenye Ofisi ya Mkuu wa Mkoa mjini Babati .

Ni viongozi wa Chama na Serikali wakimsikiliza Makamu wa Rais Dr. Mohamed Shein (ambae hayupo pichani ) akiwahutubia viongozi hao mjini Babati jana.

Makamu wa Rais Dr. Mohamed Shein pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Manyara Hendry Dafa Shekifu wakifurahia ngoma illiyokuwa ikichezwa ijulikanayo kama Msanja ngoma wakati wa mapokezi ya mgeni wao Mkoani Manyara –Babati

Rais Azindua ujenzi wa Barabara ya Tanga-Horohoro!!

Rais Jakaya Mrisho Kikwete(watatu kushoto), Mtendaji Mkuu wa MCC Bwana Daniel Yohannes(kushoto) na Balozi wa Marekani nchini Tanzania Alfonso Lenhardt wakishangili muda mfupi baada ya kuzindua uejnzi wa Barabara ya Tanga hadi Horohoro leo mchana.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete(watatu kushoto), Mtendaji Mkuu wa MCC Bwana Daniel Yohannes(kushoto) na Balozi wa Marekani nchini Alfonso Lenhardt(wapili) wakifunua kitambaa kwenye jiwe la Msingi kuashiria kuzindua rasmi ujenzi wa Barabara ya Tanga-Horohoro.
Baadhi ya wananchi wa eneo la Mikocheni Tanga wakisalimiana na Rais Jakaya Kikwete wakati wa uzinduzi wa ujenzi wa Barabara ya Tanga Horo
barabara ya Tanga Horohoro leo mchana(picha na Freddy Maro)

MATUKIO MBALIMBALI KUTOKA MKUTANO WA ADB MJINI ABDJAN!!

Viongozi mbalimbali wa dini nchini Ivory Coast na waalikwa wengine wakisikiliza hotuba ya ufungizi wa mkutano wa 45 wa ADB jana mjini Abidjan iliyokuwa ikitolewa na Rias wa Nchi hiyo Laurent Gbagbo
ngoma ni Kikundi cha ngoma ya Temate kutoka Magharibi mwa nchi ya Ivory Coast kikitumbuiza wakati wa sherehe za ufunguaji wa mkutano wa 45 wa Benki ya Maendeleo ya Afrika(ADB) mjini Abidjan jana

Mke wa Rais wa Ivory Coast mama Simeone Gbagbo akifurahia jambo wakati wa ufunguzi wa mkutano wa 45 wa ADB jana mjini Abidjan
Picha Tiganya Vincent_ Abidjan



Rais Kikwete azindua mtambo wa kuzalisha saruji Tanga!!

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na mwananfunzi ambaye jina lake halikuweza kupatikana mara moja muda mfupi baada ya kuwasili katikaa uwanja wa ndege wa Tanga ambapo alizindua mtambo mpya wa kuzalisha saruji na kuzindua ujenzi wa Barabara ya Tanga-Horohoro.
(Picha na Freddy Maro)

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akifunua kitambaa kushiria kuzindua rasmi Mtambo Mpya wa kutengeneza Saruji katika kiwanda cha Saruji Tanga leo asubuhi.


MISS SINZA KUBEBA LAKI 500.000 VATCAN SINZA KESHO!!

Mkurugenzi wa Miss Sinza Vareria Urio akizungumza na waandishi wa habari kwenye mgahawa wa Hadees leo wakati alipokuwa akitangaza zawadi za washinda katika shindano hilo linalotarajiwa kufanyika Mei 29 jumamosi kwenye ukumbi wa Vatcan Sinza ambapo burudani itatolewa na bendi maarufu ya Fm Academia.
Mshindi wa shindani hilo atajinyakulia shilingi laki 500.000 wakati wapili atapata shilingi laki 300.000 na wa tatu ataondoka na shilingi laki 200.000 na wa nne atapata shilingi 100.000 huku kifuta jasho kikiwa shilingi 60.000 kwa washiriki wengine, kulia katika picha ni Yason Mashaka mratibu wa shindano hilo na nyuma ni warembo watakaoshiriki kwenye shindano hilo.

NDOVU SPECIAL MALT TO RECEIVE THE GRAND GOLD QUALITY AWARD 2010 IN GERMANY THIS MONTH.

The Brew Master Mr. Gaudence Mkolwe left and The Brand Manager for Ndovu Special Malt Oscar Shelukindo.

A few weeks ago we informed you that Ndovu Special Malt won a Grand Gold Quality Award 2010 from the prestigious Monde Selection, an International Body established in 1961 with the aim of awarding medals for quality to different categories of foods and drinks from various countries; beers being among them.

These awards are of four types, Bronze Award, Silver Award, Gold Award and Grand Gold Award, this being the ultimate beer rating by professional tasters of 90 to 100%,the perfect beer.

In winning a Grand Gold Quality Award, Ndovu Special Malt has only clarified what most Tanzanians have known about the beer since its launch on the 31st of September 2009.
Its taste and quality cements it as truly Tanzanians Premium Lager of choice.

It is with this in mind that we inform you that the award Ceremony will take place in Wiesbaden near Frankfurt Germany on the 31st of May 2010.

The Brew Master Mr. Gaudence Mkolwe and The Brand Manager for Ndovu Special Malt Oscar Shelukindo are scheduled to be at the 2009 Monde Selection in Wiesbaden Germany to receive the award on behalf of Tanzania Breweries and all Tanzanians.

The journey to Germany will be catalogued in various Tanzanian blogs and the return to Dar es Salaam on the 3rd of June 2010 is expected to be a big welcoming event.

Ndovu Special Malt has been recognized in a world forum of many beers and given the highest award possible, all Tanzanians should be proud of this achievement, Tanzanians are enjoying this brand in mass as they know what quality is.

ROSE JOHN NDIYE RBP MISS DAR INTER COLLEGE 2010!!

Miss RPB Dar Inter College Rose John akiwa katika picha ya pamoja na mshindi wa pili Casian Milinga kulia na mshindi wa tatu Marylidia Boniface mara baada ya kutangazwa kwa washindi katika shindano lililofanyika kwenye klabu ya Billicanas jijini Dar es salaam usiku wa kuamkia leo.
Miss RBP Dar Inter College Rose John akipingia mashabiki mkono mara baada ya kutangazwa mshindi katika shindano lililofanyika usiku wa kuamkia leo klabu ya Billicanas jijini Dar es salaam kulia ni Marylidia Boniface kushoto mshindi wa tatu na kushoto ni mshindi wa pili Casian Milinga na mwisho kulia ni Asia Idarous mwasho kushoto ni Vick Kimaro mmoja wa waratibu wa shindano hilo.
Vazi la ufukweni.

Shoo ya ufunguzi

Vazi la ubunifu.
Barnaba akiimba na msanii mwenzie katika onyesho hilo.
Mmoja wa majaji wa shindano hilo Mwandishi wa habari wa Tanzania Daima Dina Mahamoud kushoto akiongea na Mwigizaji wa kundi la Tajiquan la jijini Rehema Ndwangila aka (Loveness)wakati wa shindano la RPB Miss Dar Inter College lililofanyika jana kwenye klabu ya Billicanas jijini Dar es salaam.
Majaji wa Miss Dar Inter College.
Wakuu wa kamati ya Miss Tanzania nao walikuwepo katika shundano hilo kujua kilichokua kikijiri.
Mbunifu wa mavazi Asia Idarous wa tatu kutoka kulia akiwa katika picha ya pamoja na wanamitindfo wake kushoto ni Mwigizaji wa kundi la Tajiquan Rehema aka Loveness.
Wapenzi mbalimbali wa urembo wakifuatilia shindano la Miss Dar Inter College.

WANANCHI MBINGA WATAKA VIGEZO VYA KUJIUNGA!


Na Mohammed Mhina, wa Jeshi la Polisi

Wananchi wa Mikoa ya Kusini mwa Tanzania wameiomba Serikali kupitia Wizara ya Mambo ya ndani kuangalia upya vigezo vya ajira kwa Jeshi la Polisi vinavyozingatia urefu ili kutoa nafasi kwa vijana wasio na sifa hizo kunufaika na ajira kwenye Jeshi la Polisi.

Wananchi hao wametoa ombi hilo kwa Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini Inspekta Jenerali Saidi Mwema, wakati wa ziara yake ya wiki moja mkoani Ruvuma ambapo wamesema kuwa kufuatia kigezo cha urefu, kimewafanya vijana wengi wa Mikoa hiyo kukosa nafasi ya kuajiriwa kwenye chombo hicho hata kama wanaviwango vikubwa vya ulemu na ujuzi mbalimbali.

Akizungumza katika mkutano huo, mkazi mmoja wa wilaya ya Mbinga mkoani Ruvuma Bw. Joseph Mapunda, amesema kuwa, kwa muda mrefu sasa, vijana wa mikoa ya Ruvuma, Mtwara na Lindi ambao wengi wao ni wafupi wakilinganishwa na vijana wa mikoa mingine hapa nchini, wamekuwa wakikosa nafasi za ajira katika Jeshi hilo na Majeshi mengine kutokana na maumbile yao.

Amesema baadhi ya vijana waliokuwa wakiomba kujiunga na majeshi ya ulinzi na usalama hapa nchini wamekuwa wakiambulia patupu kutokana na kikwazo hicho pamoja na kwamba wana nia na ari ya kulitumikia taifa lao ndani ya Majeshi hayo. Hata hivyo IGP Mwema, amesema nia ya Jeshi la Polisi ni kuajiri askari kutoka katika kila wilaya na mikoa hapa nchini kwa lengo la kuwa na Jeshi lenye sura ya Kiataifa na kwamba kigezo cha urefu kitatazamwa upya hasa kwa baadhi ya vijana wa maeneo ya mikoa ya kusini mwa Tanzania.

Amesema kwa kufanya hivyo, kutatoa fursa kwa vijana wengi wa Kitanzania wenye elimu inayotajwa kwenye sifa za ajira katika majeshi yetu kuweza kujiunga. Katika hatua nyingine Mkuu huyo wa Jeshi la Polisi nchini ametoa wito kwa Watanzania kutumia haki yao ya Kikatiba katika uchaguzi Mkuu ujao baadaye Oktoba mwaka huu kwa kuwachagua viongozi wanaodhani kuwa wataliongoza taifa letu kwa amani na utulivu.

IGP Mwema alikuwa akizungumza katika mikutano tofauti huku akinadi katika wilaya alizozitembelea mkoani Ruvuma na huku akinadi kitabu cha wajibu wa mpiga kura kilichoandaliwa na Jeshi la Polisi nchini kama dira kwa Watanzania kuelekea uchaguzi mkuu ujao hapo baadaye mwaka huu.