Furguson ajadiliwa na FA kuhusu refa!!

Meneja wa Manchester United Alex Ferguson.

Chama cha soka cha England- FA kimethibitisha kitashughulikia malalamiko ya meneja wa Manchester United Alex Ferguson kwa mwamuzi Alan Wiley juu ya mchezo wa mwishoni mwa wiki.
Ferguson alishutumu kiwango cha uwezo wa mwamuzi Wiley wakati akichezesha mchezo baina ya Manchester United na Sunderland, ambapo timu hizo zilitoka sare ya mabao 2-2.
Furgeson amesema:"Hali ya mchezo ule ilikuwa inahitaji mwamuzi aliye imara. Huyu hakuwa imara. Ilikuwa ovyo".
Nayo malalamiko ya meneja wa Blackburn Sam Allardyce kwa mwamuzi Peter Walton baada ya timu yake kulazwa na Arsenal siku ya Jumapili yatajadiliwa.
Sam Allrdyce alitoa malalamiko baada ya timu yake kuzabwa mabao 6-2 na Arsenal, ambapo mwamuzi alishindwa kutoa adhabu ya mkwaju wa penalti baada ya mlinzi wa Arsenal Thomas Vermaelen akionekana kumbana na kumwangusha David Dunn wakati huo matokeo yakiwa 3-2. na http://www.bbcswahili.com/

Serikali imetoa jumla ya tani 372.4 za chakula kwa wilaya ya Bagamoyo ili kuweza kukabiliana na tatizo la njaa!!

Waziri wa Kilimo na Chakula Steven Wassira
Na Anna Nkinda – Maelezo, Bagamoyo
05/10/2009 Serikali imetoa jumla ya tani 372.4 za chakula kwa wilaya ya Bagamoyo ili kuweza kukabiliana na tatizo la njaa linaloikabili wilaya hiyo.
Hayo yamesemwa jana na Mkuu wa wilaya hiyo Magessa Mulongo wakati akieleza hali ya chakula kwa mke wa Rais Mama Salma Kikwete wakati wa ziara yake ya kikazi ya siku moja katika wilaya hiyo .
Mulongo alifafanua kuwa tani 186.2 ziligawiwa bure kwa wananchi na tani 186.2 zilitolewa kwa utaratibu wa kuuza ambapo kilo moja iliuzwa Tshs.50.
“Vijiji 64 kutoka katika kata 16 zenye jumla ya watu 132,703 wameombewa msaada wa chakula kupitia TASAF kwa mradi wake wa uhakika wa chakula (FOOD Security)”, alisema.
Alizitaja sababu za wilaya hiyo kukabiliwa na njaa kuwa ni kutokana na mavuno hafifu msimu wa kilimo 2008/2009 kwani wilaya hiyo ina upungufu wa chakula cha mizizi na nafaka tani 39,270 na mikunde tani 6,356.
Eneo lenye upungufu mkubwa wa chakula linajumuisha kata za Msata, Mbwewe, Kibindu, Miono, Mkange, Lugoba, Ubena, Chalinze na Tawalanda ambako kuna waathirika 112,144 na eneo lenye upungufu wa kati wa chakula linajumuisha kata za Vigwaza na Kiwangwa zenye waathirika 14,846.
Mkuu huyo wa wilaya aliendelea kutaja eneo lenye upungufu kidogo wa chakula ambalo linajumuisha kata za Dunda, Magomeni, Yombo, Kiromo na Zinga zenye waathirika 15,550 na kufanya jumla ya waathirika wote kuwa ni 142,540 sawa na asilimia 53 ya wakazi wote.
Kwa upande wake Mama Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) aliwataka wakazi wa wilaya hiyo kutunza chakula walichonacho na kutokiharibu wakati wa sherehe za kuwacheza ngoma watoto wao.
“Siwakatazi kucheza ngoma, ngoma chezeni lakini muwe na matumizi mazuri ya chakula kwani mkiangalia hali halisi hivi sasa wilaya hii inkabiliwa na njaa hivyo basi kuna haja ya kutunza chakula kilichopo”, alisema Mama Kikwete.

WACHEZA FILAMU CHIPUKIZI KUSAKWA TANZANIA!!

Mchakato wa kutafuta na kuibuwa vipaji vya waigizaji chipukizi linaanza rasmi na litahusisha mikoa ya Arusha, Mwanza, Mbeya, Dodoma, Zanzibar na Dar es Salaam.
Uibuaji na ukuzaji wa vipaji vya wasanii chipukizi wa filamu ambao hawajawahi kushiriki katika filamu au tamthilia yoyote itawahusisha watanzania wenye vigezo vya kuwa na umri wa miaka 16 na kuendelea, awe na akili timamu, awe ni raia wa Tanzania na ajue kusoma na kuandika.
Mchakato utahusisha kufanya usaili katika mikoa husika hadi watakapopatikana kumi bora ambapo washiriki watachuana kumtafuta msanii chipukizi wa filamu Tanzania.
Mwaka huu kampuni mbali mbali zimejitokeza kudhamini mashindano haya lakini yatatajwa hapo baadaye
Mshindi wa IBUA Film Star Tanzania atajinyakulia zawadi ambayo itatangazwa baadae na pia atapata mkataba wa kushiriki filamu mbali mbali za wasanii wa ndani na nje ya nchi.
Mshindi atapatikana kwa kupigiwa kura na wananchi kupitia kipindi maalumu kitakachoonyeshwa hapo baadae.
Fomu za kushiriki shindano la IBUA Film Stars Tanzania zinapatikana mikoa husika kama ifuatavyo Arusha (Club Silk), Mwanza (Salma Cone), Mbeya (CPMTL Stationery mkabala na ofisi ya mkuu wa mkoa), Dodoma (Zunny Ice Cream Parlour), Zanzibar (Ofisi za Zenj FM), Dar es Salaam (TCC Chang’ombe, Shear Illusions mlimani City, Royal Salon Sinza, Zizzou Fashions). Fomu zitaanza kupatikana tarehe 10 Oktoba 2009.
Mwisho wa kuchukua fomu ni tarehe 30 Oktoba 2009 kabla ya kuanza usaili mjini Arusha tarehe 31 Oktoba na 01 Novemba.
Zoezi la usaili litafanyika kabla ya wananchi kupata nafasi ya kutoa maoni na kufanikisha kuwapata washindi.
Jacqueline Wolper
Afisa Uhusiano-YEC PRODUCTION

TUJENGE URAFIKI NA VIJANA WETU.

Brother Geffy akiwa ametulia na Kijana wake ,Hapo ni mitaa ya Makumbusho DSM.

Rais Kikwete aliporejea Dar kutoka Mwanza

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam William Lukuvi muda mfupi baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa dar es Salaam akitokea Mwanza ambapo alikuwa mgeni rasmi katika sherehe za kuadhimisha mika mia moja tangu kuanzishwa kwa kanisa la Africa Inland church Tanzania zilizofanyika katika uwanja wa michezo wa Kirumba jijini Mwanza leo(picha na Freddy Maro)

FIESTA 2009 SHOW LOVE INAHAMIA MKOANI MWANZA WAKAZI WA HUKO KAENI MKAO KUSHANGWEKA OKTOBA 10!!

Mkurugenzi wa Radio Clouds Fm na Prime Time Promotions Joseph kusaga akizungumza na wasanii kutoka nchini Uganda, mara baada ya kufanya vyema katika tamasha la fiesta usiku wa kuamkia leo tamasha hilo litaendelea huko Mkoani Mwanza ambapo wasanii kibao watashoo Love tarehe 10 oktoba wakazi wa mwanza kaeni mkao wa kushangweka.
Alikiba akiimba jukwaani kwenye tamasha la fiesta one love 2009,lililofanyika jana usiku katika uwanja wa hotel ya equitor,mjini Arusha.Baada ya kufanyika mjnii Arusha tamasha la fiesta linaelekea jijini Mwanza ambapo litafanyika wiki ijayo (jmosi)

Rais Kikwete ahudhuria sherehe za miaka mia moja ya Africa Inland Church Mwanza!!

Askofu Mkuu wa kanisa la Africa Inland Chiurch Tanzania Mhashamu Danieli Nungwana akimkaribisha Rais Jakaya Mrisho Kikwete katika uwanja wa michezo wa Kirumba ambapo Rais Kikwete alikuwa mgeni rasmi katika sherehe za maadhmisho ya miaka mia moja ya tangu kuanzishwa kwa Kanisa la Africa Inland Church Tanzania leo asubuhi(Picha na Freddy Maro)
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimianan na baadhi ya Maaskofu wa kanisa la African Inland Church Tanzania(AICT) muda mfupi baada ya kuwasili katika uwanja wa michezo wa Kirumba, jijini Mwanza ambapo alikuwa mgeni rasmi katika maadhimisho ya miaka mia moja tangu kuanzishwa kwa kanisa hilo nchini Tanzania
Baadhi ya wananchi waliohudhuria sherehe za maadhimisho ya miaka mia moija tangu kuanzishwa kwa kanisa la Africa Inland Church Tanzania leo katika uwanja wa michezo wa Kirumba jijini Mwanza leo asubuhi

Wanafunzi 287 wapata ujauzito kwa kipindi cha miezi tisa mkoani Pwani!!

Hajati Amina Mrisho Said Mkuu wa Moa wa Pwani
Na Anna Nkinda – Maelezo, Kibaha

04/10/2009 Jumla ya wanafunzi 287 wamepata ujauzito kwa kipindi cha miezi tisa katika mkoa wa Pwani na hivyo kushindwa kumaliza elimu ya msingi na sekondari.
Hayo yamesemwa jana na Mkuu wa Mkoa huo Hajati Amina Mrisho Said wakati akisoma taarifa ya maendeleo ya mkoa kwa mke wa Rais Mama Salma Kikwete aliyetembelea shule ya Sekondari Magindu iliyopo wilayani Kibaha kwa ajili ya kutoa msaada wa magodoro 100 na vitanda vitanda vyake.

Hajati Amina alisema kuwa wilaya ya Rufiji inaongoza kwa kuwa na idadi kubwa ya wanafunzi waliopata ujauzito kwani kuanzia Januari hadi Septemba mwaka huu wanafunzi 130 wamepata ujauzito ambapo wanafunzi wa Shule ya Msingi ni 110 na Sekondari ni 20.Aliitaja wilaya ya Mafya kuwa haina tatizo kubwa la wanafunzi kupata ujauzito ukilinganisha na wilaya zingine kwani kwa mwaka huu waaunzi wa shule ya Msingi watatu na sekondari kumi ndio waliopata uajauzito.

VODACOM MISS TANZANIA 2009 NI MAGEUZI MAKUBWA,MREMBO KUTOKA MWANZA ABEBA TAJI TENA!!

Vodacom Miss Tanzania Miriam Gerald ambaye ni miss Mwanza pia akipungia mashabiki wake mkono mara baada ya kutangazwa mshindi kartika shindano lililofanyika jana kwenye ukumbi wa Mlimani City na kushirikisha warembo wapatao 29 hivi baada ya mmoja wao kutolewa katika shindano hilo kutokana na kugundulika kuwa ni mjamzito.
Mkoa wa Mwanza kwa mara ya pili umetoa mrembo wa Tanzania na kudhihirisha uwezo wake katika mashindano hayo makubwa na yenye mvuto nchini, Miriam anachukua nafasi ya Vodaciom Miss Tanzania 2008 Nasreem Karim ambaye pia alitokea mkoani mwanza na kuufanya mkoa huo kuzichachafya kanada za Mkoa wa Dar es salaam Ilala Temeke na Kinondoni ambazo mara nyingi zimekuwa zikijitapa kuwa ndizo zenye warembo bomba kitu ambacho kimedhihirisha kuwa Tamb zao ni hazimzuii tembo kutoka Mwanza kunywa maji kisimani.
Miriam Gerald FULLSHANGWE inakutakia kila mafanikio katika kazi zako zote za Miss Tanzania ni kazi ngumu lakini ukiwa makini, ukajiheshimu na kusikiliza ushauri utashinda majaribu yoyote katika kazi hizo Mungu akujalie sana

Vodacom Miss Tanzania 2009 Miriam Gerald akiwa katika gari yake aina ya Suzuki Grand Vitara mara baada ya kukabidhiwa baada ya kushinda taji hilo,

Vodacom Miss Tanzania Miriam Gerald akiwa katika picha ya pamoja na washindi wengine mara baada ya majaji kutangaza washindi kwenye shindano lililofanyika usiku wa leo kwenye ukumbi wa Mlimani City kulia ni Beatrice Lukindo mshindi wa pili na kushoto ni Julieth miki mshindi wa tatu.

Mrembo miriam Gerald akishangilia mara baada ya kuibuka mshindi wa taji la Vodacom Miss Tanzania katika shindano lililofanyika kwenye ukumbi wa Mlimani City usiku wa kuamkia leo jijini Dar es salaam.

Mewa Bodi ya Utalii nchini Geofrey Meena akmvisha taji la Ubalozi wa Utalii nchini mrembo Sia Ndeskoi

Naibu Mkurugezi wa Utafiti na Mafunzo Wizara ya Maliasili na Utalii Ibrahim Mussa akitangaza mshindi aliyejinyakulia taji la Utalii lililotolewa na Bodi ya Utalii nchini TTB kulia Meneja Masoko wa bodi hiyo Geafrey Meena akishuhudia tukio hilo.

Mkurugenzi wa masoko wa kampuni ya Bia TBL David Minja akimkabidhi zawadi yake mrembo Miriam Gerald mara baada ya kutangazwa kuwa Redds Miss Photogenic jana. kulia ni meneja wa kinywaji cha Redds Kabula Nshimo akishuhudia tukio hilo.

Baadhi ya majaji wakiongozwa na Mwenyekiti wa kamati ya Miss Tanzania Prashant Patel katikati wakijumulisha matokea ya mwisho ili kumpata mrembo wa Vodacom Miss Tanzania kazi iliyofanywa kwa ufasaha na umakini.

Hii ndiyo Tano bora mara baada ya kutangazwa na hapa wakijiandaa kwa maswali.

Hapa baadhi ya warembo wakipita na vazi la jioni.

Baadhi warembo wakipita jukwaani na vazi la ufukweni

Naye Ray C. akamwaga uno na kulizungusha kama pia kama ilivyo kawaida yake.

Vijana hawa kutoka Nchini Uganda nao walifanya mambo makubwa kutokana na uwezo walionao katika kuimba na kutawala jukwaa,mara nyingi wanamuziki kutoka uganda wamekuwa na uwezo mkubwa katika muziki ukilinganisha na wanamuziki wengine kutoka nchi za Afrika Mashariki.

THT kama kawaida ya wakafanya makamuzi makubwa jukwaani hili ni kundi la kuigwa kwakweli wadau.

Mzee Zahir Ally Zorro akifanya vitu vyake jukwaani.

Mdau Muddy kushoto na rafiki yake pia hawakutaka kukosa kinyang'anyiro hicho pale mlimani City.
Mboni Masimba kushoto na rafiki yake Joan na rafiki yao wakitaka kujua
mambo yanavyokwenda

Kijana Komu wa TBCI akishoLove na Lisa Jensen kushoto na Jaquiline Patrick amani na upendo daima.

Jokate Mwegelo kushoto akiwa na rafiki zake Natalie na Elsi.

Mkurugenzi wa Aset Asha Baraka akiwa na Meneja wa kinywaji cha Kilimanjaro Lager George Kavishe.

Mdau wa Simba Nick Butt na maiwaifu wake kulia na Mdau Rodrick Mwambene aliyekaa nyuma na maiwaifu wake kushoto wakipozi mbele ya Camera ya FULLSHANGWE.

Mgeni Rasmi katibu mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii Dr. Ladislaus Komba kulia, Ibrahim Mussa Naibu Mkurugenzi wa Utafiti na mafunzo Bodi ya Utalii na aliyekuwa mkurugenzi wa Africa Media Group Franco Tramontana wakifuatilia kwa karibu wakati shindano hilo lilipokuwa likiendelea jana.

Mamaa Shamimu Zeze wa www. 8020fashions.blogpot.com akiwa katika picha ya pamoja na Jaquilene Ntuyabaliwe na mwanamitindo Flaviana Matata
katikati
Meneja Masoko Multchoice Furaha Samalu kushoto akiwa na rafiki ya Garina.

Mercy Galabawa kulia Fina Mango kati na Sofia Byanaku wakifuatilia shinfdano hilo jana.

JK AFUNGUA MKUTANO WA BUNGE LA JUMUIYA YA MADOLA CPA ARUSHA!!

Rais Jakaya Kikwete amewasili leo asubuhi iwanja wa ndege wa KIA jijini Arusha kufungua mkutano wa 55 wa bunge la jumuiya ya Madola CPA unaofanyika katika ukumbi wa AICC kushoto kwake ni Rais wa CPA na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Spika Samwel Sitta, Mkuu wa mkoa wa Arusha Isdore Shirima, Katibu wa Bunge Dk Kashilila na kushoto ni Naibu Waziri wa mambo ya nje Balozi Seif walipomlaki uwanjani hapo

BIG BROTHER AFRICA REVOLUTION - Daily Updates - Day 25 (October 1, 2009)

Kaone.

Day 25 of M-Net’s BIG BROTHER REVOLUTION was a shocker – in more ways than one! Make-ups, breakups and staying awake dominated the housemates’ time, though ultimately they lost their first task of the Revolution – and therefore 50% of their budget for next week. The ladies teamed up with Kevin, Kaone, Quinn, Itai and Jeremy to create a stronger opposing alliance to the Smokers’ Alliance. Itai got in trouble for revealing details of that alliance’s plans to Yacob and having failed to undo the damage he did, has switched allegiances to the “Smokers”. Now the women have no idea who to trust and the alliances seem to be teetering. Hannington told Big Brother that the scheming in the house has brought out his dishonest side – which he doesn’t like - and so has declared that he is ‘over’ alliances, while Kristal also told Koane and Kevin that she is now flying solo as she trusts no one.
The task for the day included a giant “Pillow Fight” which saw the housemates fighting to knock each other off the giant bed in the garden with oversize pillows, “Wisdom and Learning” which saw one housemate at a time reading a supplied page from an encyclopedia while the other housemates acted out what they were hearing and “Stun Buzz”, where the housemates were asked to don special suits and guide a metal handle with a circular end through an intricate twisted pathway without allowing the two to touch.

Baada ya kupata ajali amesahaulika, hakuna uduma ya matibabu, wadau tumsaidie Mwanamziki huyu!

Hamisi Kitambi ni mmojawapo wanamziki wakongwe na hadhina waliobakia hapa nchini Tanzania ,bwana Hamisi Kitambi mtunzi wa nyimbo nyingi !mojawapo ya nyimbo zake ni ule wimbo mzuri maarufu kwa jina " Mpenzi wangu !mwenye rangi ya Chungwa" kwa wale wenye kumbukumbu wanajua radha ya utamu wa wimbo huo..veteran huyu Hamisi Kitambi amefanya kazi na bendi nyingi zikiwamo Tabora jazz,Unyanyembe band,penginepo KIKO KIDS,labda Dar-es-salam Jazz,labda Western Jazz, hadi anapata ajali ya gari alikuwa Juwata (OTTU) Jazz sasa Msondo Ngoma aka Baba ya Mziki.
Mwanamziki huyu mkongwe Hamisi Kitambi amepata hajali akiwa katika gari yeye na wanamziki wenzie Msondo Ngoma walipokuwa safarini Tanga! Mzee Hamisi Kitambi kama anavyoonekana pichani,miguu imevunja na amewekewa vyuma,cha kusikitisha kuwa tangu apate hajali ndio katupwa si ,hana uduma muhimu,mtaji wa masikini ni MIGUU YAKE nayo ndio kama anavyoonekana,Je ! ni haki kwa mwanamziki au mwanadamu aliyechangia kujenga msingi wa fani ya mziki nchini kutupwa kama hivi?Basi ata kama hakuna bima ya kulipwa,ata ubinadamu usiwepo?Tujaribu kumsaidia mzee wetu huyu mwanamziki mkongwe Hamisi Kitambi anapatikana kwa simu hii Dar 0713576475

Xavi wants Fabregas at Barça

Barcelona midfielder Xavi

Barcelona midfielder Xavi has risked infuriating Arsenal by expressing his ambition to play with Cesc Fabregas at Camp Nou, and claiming his Spain team-mate has "Barça DNA".
The Gunners captain started his career at the Catalan giants before Arsene Wenger recruited him as 2003 as a 16-year-old, but he has consistently been linked with a return to La Liga since establishing himself in the Premier League.
As the player of the tournament at UEFA EURO 2008 and a key component of Barcelona's treble-winning team last season, Xavi is viewed as an influential figure at his club and his comments could be seen as increasing pressure on Fabregas to move. "I'd like to play with him,' the 29-year-old told Spanish newspaper El Mundo Deportivo.

He is a player with Barça DNA and is showing at Arsenal that he is on another level. I would love him to sign so that we could play together.
Xavi on his desire to see Cesc Fabregas join him at Barcelona
"I've always said that in the national team I link up with Cesc very well, despite the fact that many say we can't play together. We demonstrated in the final of the European Championship that isn't true.
"I especially hope that Cesc comes. He is a football player with Barça DNA and he is showing at Arsenal that he is on another level. I would love him to sign so that we could play together at Barça. Clearly, a lot of his career is ahead of him and I think that in the future it will be at Barça."
Job for lifeWenger has dealt with speculation about Fabregas in previous seasons and will be hoping a transfer saga does not sour his 13th year in charge, making him Arsenal's longest-serving manager. Gunners director Ken Friar has suggested the Frenchman has a job for life at the club.
"We will all be very, very sad when the day comes when Arsene decides he's had enough," he said on the club's official website. "We will never have enough of him and he will be welcome here with his lovely wife and daughter forever.
"They are now part of the club's history. Arsene has engraved himself on the club forever and that I think is the greatest tribute to anybody. The fact that, no matter how many years go by, Arsene will always be remembered. That cannot be said about many people."
Wenger's appointment in 1996 was seen by some as a risk by some, but not Friar. "I suppose we are relatively risk-averse but we did not feel that we were taking such a big gamble on Arsene," he said.
"He'd done well at Monaco - he'd won the French title there, he was French manager of the year - so he wasn't a complete rookie coming off Hackney Marshes." story by www.fifa.com

SERA YA MAJI YAJADILIWA NA WADAU WA MAJI NA TAASISI ZAKE!!

Waziri wa Maji na Umwagiliaji Prof. Marck Mwandosya akizungumza na waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali mara baada ya kufungua warsha ya Mkakati wa pamoja wa kuangalia upya sera ya maji iliyoanza leo katika jengo la Ubungo Plaza jijini Dar es alaam, Warsha hiyo inashirikisha wadau mbalimbali wa maji na Taasisi zake na itaendelea mpaka kesho.
Washiriki mbalimbali wa warsha ya Mkakati wa pamoja wa kuangalia upya sera ya maji inayofanyika leo Ubungo Plaza jijini Dar es salaam wakisikiliza kwa makini wakati Waziri wa maji na umwagilaji Prof Marck Mwandosya alipokuwa akifungua warsha hiyo leo.


TAMASHA LA 28 LA SANAA BAGAMOYO LAENDELEA!!

Wasanii wa kikundi cha sanaa cha Kimanzichana wakicheza ngoma ya uwindaji ya ukala wakati wa Tamasha la 28 la sanaa za utamaduni wa Tanzania linaloendelea Bagamoyo hii ilikuwa ni usiku wa kuamkia leo.

Kenya Commercial Bank yawapa somo la ujasiriamali warembo Miss Tanzania!!

Meneja Masoko na Mawasiliano wa Kenya Commercial Bank, Christina Manyenye akizungumza na washiriki wa shindano la Vodacom Miss Tanzania 2009 wakati wa semina na warembo hao kuhusu masuala ya ujasiriamali kambini kwao Hoteli ya Giraffe, Dar es Salaam jana.
Warembo wanaowania taji la Vodacom Miss Tanzania wakiwa kwenye picha ya pamoja na wafanyakazi wa KCB Benki tawi la mlimani city,Kesho ndiyo watamenyana rasmi.