Furguson ajadiliwa na FA kuhusu refa!!

Meneja wa Manchester United Alex Ferguson.

Chama cha soka cha England- FA kimethibitisha kitashughulikia malalamiko ya meneja wa Manchester United Alex Ferguson kwa mwamuzi Alan Wiley juu ya mchezo wa mwishoni mwa wiki.
Ferguson alishutumu kiwango cha uwezo wa mwamuzi Wiley wakati akichezesha mchezo baina ya Manchester United na Sunderland, ambapo timu hizo zilitoka sare ya mabao 2-2.
Furgeson amesema:"Hali ya mchezo ule ilikuwa inahitaji mwamuzi aliye imara. Huyu hakuwa imara. Ilikuwa ovyo".
Nayo malalamiko ya meneja wa Blackburn Sam Allardyce kwa mwamuzi Peter Walton baada ya timu yake kulazwa na Arsenal siku ya Jumapili yatajadiliwa.
Sam Allrdyce alitoa malalamiko baada ya timu yake kuzabwa mabao 6-2 na Arsenal, ambapo mwamuzi alishindwa kutoa adhabu ya mkwaju wa penalti baada ya mlinzi wa Arsenal Thomas Vermaelen akionekana kumbana na kumwangusha David Dunn wakati huo matokeo yakiwa 3-2. na http://www.bbcswahili.com/

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment