Katika Kijiji cha Halukumbi Tarafa ya Katunguru kata Chifunfu wilayani Sengerema wanafunzi 18 kati ya 37 waliokuwa wakisafiri ziwani Victoria kwa Mtumbwi kwenda shule leo asubuhi majira ya saa 1:45 walizama na kufa maji. Mpaka sasa miili 12 ya watoto hao waliokufa imekwsiha patikana huku mingine 6 ikiendelea kutafutwa ndani ya ziwa.
Akihojiwa kwa njia ya simu na shirika la Utangazaji la Taifa TBC Kamanda wa polisi wa mkoa wa Mwanza Kamanda Simon Silo amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo katika ziwa Victoria na juhudi za kutafuta miili zaidi ya watoto hao zinaendelea.
Lakini pia Mwandishi wa jeshi la polisi Mohamed Muhina amemkariri Kamanda wa polisi Mkoa wa Mwanza akithibitisha kutokea kwa tukio hilo.
0 comments:
Post a Comment