Na Mohammed Mhina, wa Jeshi la Polisi
Jeshi la Polisi nchini limesema kuwa limeandaa mazingira mazuri yatakayomuwezesha kila Mtanzania mwenye haki ya kupiga kura anafanya hivyo kwa uhuru, usalama na amani.
Kauli hiyo imetolewa leo na Mkuu wa Hudunma za Polisi Jamii nchini Naibu Kamishna wa Polisi DCP Isaya Mngulu. wakati akizungumza na Wanafunzi na Wakufunzi wa Tanzania Polisi Academy Kurasini Jijini Dar es salaam.
Amesema kuwa Jeshi hilo limetoa kitabu kwa ajili ya kusaidia kutoa elimu kwa askari na wananchi juu ya wajibu wa kila mmoja kwa upande wake wakati wa kampeni na uchaguzi mkuu uliopangwa kufanyika mwezi Oktoba mwaka huu.
Amesema tayari Jeshi la Polisi limechapichasha nakala 30,000 za kitabu kijulikanacho kama haki na wajibu wa mpigakura ambapo kimeelezea pia wajibu wa Askari Polisi wakati wa mchakato wa kampeni, kupiga kura, kuhesabu na kutangaza matokeo.
DCP Mngulu amesema kuwa kwa kushirikiana na UNDP Jeshi hilo litahakikisha kuwa vitabu hivyo vinasambazwa na elimu kutolewa kwa kila mpigakura kwa njia ya mikutano na kuvigawa kwa mtu moja moja.
Aidha DCP Mngulu pia amesema kuwa Jeshi la Polisi litasambaza askari wawili wawili kwenye kila kata hapa nchini na kwamba vituo vya Polisi vilivyopo kwenye tarafa sasa vitaongozwa na askari wenye vyeo vya kuanzia Inspekta badala ya Sajenti na Sajinimeja.
Naye Mkuu wa Nidhamu wa Tanzania Police Academy SP Loydi Mussa, amesema kuwa askari wanaohudhuria mafunzo kwenye chuo hicho wanajengewa uwezo wa kukabiliana na matukio makubwa ikiwa ni pamoja na migomo mbalimbali.
DCP Mngulu ambaye pia ametembelea na kuona hali mbaya ya baadhi ya nyumba za za Wakufunzi wa Tanzania Police Academy, ameelezwa kuwa chuo hicho kina uhaba mkubwa wa makazi na kwamba baadhi yao wanaishi kwenye magofu.
0 comments:
Post a Comment