NA MAGRETH KINABO NA BENJAMIN SAWE – MAELEZO
SERIKALI imetoa sh. bilioni 103 kwa ajili ya kupeleka umeme vijijini chini kupitia Wakala wa Nishati Vijijini(REA) ambayo itatekelezwa katika mikoa 16 , ukiwemo ya mingine ya Liliondo na Kishapu.
Haya yalisemwa jana Bungeni na Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja wakati akitoa kauli ya Serikali kuhusu utekelezaji wa miradi mipya ya kupeleka umeme vijijini inayofadhiliwa na Serikali kupitia REA, Millenia Challenge Corporation(MCC), Benki ya Maendeleo ya Afrika(AfDB) na Serikali ya Sweden(SIDA).
Alisema kati ya fedha hizo sh. bilioni 98.4 zitatumika katika mkioa hiyo,na fedha zilizobakia ni kwa ajili ya miradi ya Loliondo na Kishapu. Waziri Ngeleja aliitaja mikoa hiyo itakayotekelezewa miradi ni Arusha,Kilimanjarao, Manyara, Tanga, Pwani, Morogoro, Dodoma, Singida, Mbeya, Rukwa, Tabora, Kigoma, Kagera Mwanza, Mara na Shinyanga.
Miradi hiyo itahusisha ujenzi wa njia za umeme zenye msogo wa kilovolti 33 pamoja na 11zenye jumla ya takribani kilometa 1600,ufungaji wa transfoma 350 za ukubwa tofauti, ujenzi wa bnjia za umeme wa msongo wa kilovolti 0.4 zenye jumla ya kilometa 90o, uunganishaji wa watejawapya wanaokadriwa kufikia 20,000. Alisema usmamizi wa utekelezaji wa miradi hiyo utakuwa chini ya Shirika la Umeme Tanzania(TANESCO).
Waziri Ngeleja alisema utekelzaji wa miradi ya kupeleka umeme makao makuu ya wilaya ya Ngorongoro(Loliondo) na mkoa wa Arusha utafanywa na TANESCO ingwa wanaweza kushirikiana na sekta binafsi.
0 comments:
Post a Comment