MGOMBEA UBUNGE DEWJI ANUSURIKA KIFO..!!!!


Na Hillary, Shoo,Singida.


Mgombea Ubunge wa Jimbo la Singida Mjini CCM, Mohammed Dewji(MO) jana amenusurika kifo baada ya gari alilokuwa akisafiria kutoka katika kampeni kugongwa kwa nyuma na gari alilokuwa akitumia mgombea mwenzake Hawa Ngulume kuligonga kwa nyuma basi hilo dogo.



Ajali hiyo imetokea jana majira ya saa 10 jioni katika eneo la ofisi za Manispaa ya Singida muda mfupi baada ya wagombea hao kutoka katika kata ya majengo kunadi sera zao kwa wanachama kwa ajili ya kuwania kuteuliwa kuwa mbuunge wa jimbo hilo ambalo MO alikuwa mbunge aloiyemaliza muda wake.



Kwa mujibu wa watu walioshuhudia tukio hilo walisema kuwa katika hali isiyokuwa ya kawaida walipatwa na mshangao mkubwa baada ya kuona dreva wa gari aina ya Land Cruiser lenye namba za usajili T 425 AMK ambaye jina lake bado halijahafahamika kugonga HIACE hiyo yenye namba za usajili T 655 BEB iliyokuwa ikitumiwa na Dewji pamoja na mwenzake aitwae Mariam Mhuwila.



Habari zaidi zinasema kuwa juzi wagombea wote Dewji, Mariam na Ngulume walipanda gari moja lakini jana Ngulume alikataa kupanda gari hilo maalumu kwa ajili ya wagombea na kuamua kutumia gari lake binafsi.Katika ajali hiyo Dewji alipata mshituko sehemu ya shingo baada ya gari hilo kugomga kwa nyuma Hiace hiyo ambapo MO alikuwa amekaa nyuma na kusababisha kupata majeraha na mshituko sehemu ya shingo na kukimbizwa katika hospitali ya mkoa kwa ajili ya matibabu.



Hata hivyo baada ya kufanyiwa uchunguzi wa vipimo vya X ray ilibainika kuwa MO amepata mshituko sehemu ya shingo na kupatiwa dawa za kuchua kabla ya kuruhusiwa kurejea nyumbania na hali yake inaendelea vizuri.Kufuatia ajali hiyo dereva wa Mgombe hawa Ngulume anahojiwa na polisi kwa tuhuma ya kuendesha gari kizembe na kusababisha ajali.Kamanda wa polisi Mkoani hapa Celina Kaluba amethibitisha kutokea kwa ajili hiyo na kwamba uchunguzi bado unaendelea kuhusiana na tukio hilo na taarifa kamili zitatolewa leo ili hatua zaidi ziweze kuchukuliwa kwa wahusika.



Juhudi za kumpata Katibu wa CCM Manispaa ya Singida Mary Maziku ili kuzungumzia tukio hilo hazikufanikiwa hadi tunakwenda mitamboni.Nashukuru kwa Ushirikiano wenu wadau wote.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment