Mbio za kuelekea katika kinyang’anyiro cha kumsaka mlimbwende wa kanda ya kaskazini zimezidi kupamba moto katika kambi ya warembo wanaoshiriki kinyang’anyiro hicho kutoka mikoa ya Arusha, Kilimanjaro, Manyara na Tanga.
Shindano hilo litakalofanyika Ijumaa Julai 16, 2010 katika hoteli ya kitalii ya Naura Springs iliyopo Jijini Arusha limeanza kuwa gumzo kufutia ushindani wa warembo uliopo.
Warembo wa Miss Northern Zone 2010 wanaojifua chini ya Densa maarufu nchini Bob Richie katika hoteli ya City Link iliyopo pembeni kidogo ya Mji wa Arusha eneo la Kimandolu wapo katika hari kubwa kila mmoja akijinasibu kumfunika mwenzie.
Erasto Jones ambae ni Mkurugenzi wa Shindano hili linaloandaliwa kupitia kampuni ya Crown International Entertainment amesema mambo yote yanakwenda vizuri hadi sasa na kuwataka wapenzi wa tasnia ya urembo kanda ya kaskazini kujiandaa kushuhudia shoo ya ukweli siku ya Ijumaa.
“..Niwakaribishe kwa wingi wapenzi wote wa burudani Ijumaa hii pale Naura Springs Hotel na hii itakuwa ni burudani ya kipekee baada ya kukamilika kwa woza 2010, time for Jabulani pale Bondeni, na sasa its time for Warembo”, ametanabaisha Erasto.
Erasto ameweka bayana kuwa burudani itakayotawala usiku huo ni ya kipekee kabisa na zaidi ya yote mzee wa piiII piiii Lawrence Marima a.k.a Marlaw atawabembeleza kwa bidii wakazi wa Kanda ya kaskazini sanjari na Mshindi wa Pili wa BSS 2009/10 Peter Msechu na Vijana machachari katika dansi Hot Stone, B – Boys toka Arusha.
Viingilio kwa mujibu wa Mkurugenzi Erasto vitakuwa shilingi 30,000/= kwa V I P na shilingi 20,000/= kwa viti vya kawaida.
Miss Northern Zone 2010 inaletwa kwenu kwa udhamini wa VodaCom Tanzania, Tanzanite One, Redds Original, Naura Springs Hotel, PSI, Duka maarufu la nguo la JJ Black, Chuo cha Taifa cha Utalii kampasi ya Arusha na Hoteli ya City Link.
Wengine ni SKY Print, Studio ya kisasa ya Artful Photo Graphic, Mbunifu Maarufu wa mavazi Azizi Makoko kupitia kampuni yake ya Editions Senzia Fashion, Supreme Power Fence na Chuo cha lugha ya kifaransa Arusha Alliance Franceise.
Washindi watatu wa shindano hili ndio watakaojinyakulia tiketi za kushiriki shindano la Miss Tanzania baadae mwaka huu.
KUMEKUCHA KAMBI YA MISS NORTHERN ZONE 2010!!
Posted by
ADMIN
You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment