KATIBU MKUU WIZARA YA FEDHA KATIKA PICHA NA WAFANYAKAZI WA WIZARA HIYO!!

Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Uchumi Ramadhan Khijjah katikati akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi walioko kwenye banda la wizara hiyo katika maonyesho ya 34 ya biashara ya kimataifa yanayoendlea kwenye viwanja vya Mwalimu J.K.Nyerere jijini Dar es salaam na yanayoshirikisha kampuni kutoka nchi mbalimbali duniani.
Msemaji Mkuu wa Wizara hiyo Ingiahedi Mduma kushoto akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi mwenzake katika banda la wizara ya Fedha na Uchumi, ambapo watu mbalimbali wamekuwa wakipita na kujionea shughuli mbalimbali zinazofanywa na wizara hiyo kwa kupata maelezo kutoka kwa wataalamu kadhaa wa Wizara hiyo waliopo katika maonyesho hayo.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment