Msanii kutoka Arusha anayejulikana kwa jina la Angel ametikisa Ngome Kongwe kwa jinsi alivyonyonga kiuno kama pia, kitu kilichowafanya mashabiki kumshangilia kwa nguvu wakati akiimba jukwaani katika tamasha la Fiesta lililofanyika usiku huu mjini Zanzibar na kushirikisha wasanii wengi wa muziki wa kizazi kipya Bongofleva.
Tamasha hilo linafanyika baada ya lile la Tanga lililofanyika jumamosi kwenye uwanja wa Mkwakwani mkoani humo na linadhaminiwa na kampuni ya bia ya Serengeti Breweriers (SBL) ya jijini Dar es Salaam.
Amini naye akafanya mambo makubwa katika tamasha hilo kama unavyomuona.
Mwasiti naye hakubaki nyuma, alikamua vilivyo na kuwapambanisha mashabiki ambao aliwaita vidume (hawapo pichani), yote ikiwa ni burudani tu.
Msanii huyu pia alikuwepo na akavuta hisia za mashabiki kwa staili yake.
Mr. Wise akitoa burudani na mrembo ambaye alivuta hisia za mashabiki wengi usiku huu na kushangiliwa kwa nguvu.
Mustafa wa G5 Click akiwa kazini Ngome Kongwe.
Barnaba na Nina wakitafuta muafaka wa SMS!
Binamu Mwana FA akiwarusha mashabiki wake.
Mashabiki tofauti wakiwa ndani ya Ngome Kongwe wakishuhudia vimbwanga vya wasanii.
Hapa Mwandishi Siddy akiwa na Nina na Barnaba.
Mdau Siddy Mgumia wa pili kutoka kushoto akiwa katika picha ya pamoja na wasanii mbalimbali wa kike waliotumbuiza kwa nyakati tofauti katika tamasha la Fiesta Jipanguse mjini Zanzibar usiku huu.
Mkurugenzi wa Masoko SBL katikati akiwa katika picha ya pamoja na Teddy Mapunda wa pili kutoka kushoto, kulia ni Nandi Mwiyombela Meneja Bidhaa SBL, Mr. Mapunda anayefuata na kushoto ni Godfrey Kusaga kutoka Prime Time.
0 comments:
Post a Comment