FIESTA JIPANGUSE 2010 ILIVYOLITIKISA JIJI LA TANGA USIKU WA KUAMKIA LEO!!

Msanii maarufu Juma Nature kutoka kundi la TMK Halisi akilishambulia jukwaa katika tamasha la Fiesta Jipanguse 2010 lililofanyika usiku wa kuamkia leo kwenye uwanja wa Mkwakwani mkoani Tanga na kujumuisha wasanii wengi wa muziki huo.
Tamasha hilo lilivuta hisia za mashabiki wengi na wapenzi wa muziki huo kutoka maeneo mbalimbali ya vitongoji vya mkoa wa Tanga waliokuwa wakiimbishwa kila wakati na kunyanyua mikono yao juu mara kwa mara.
Fiesta Jipanguse 2010 tayari imeshafanyika katika mikoa ya Dodoma, Morogoro, Arusha, Kilimanjaro na Tanga na leo inaendelea tena wakati itakapofanyika katika visiwa vya Zanzibar usiku wa leo, wadhamini wakuu wa tamasha hilo ni kampuni ya bia ya Serengeti Breweriers LTD.
(Picha kwa hisani ya Michuzijunior).
Meneja Mkuu wa Uhusiano, mwasiliano na Jamii wa kampuni ya Bia ya Serengeti Teddy Mapunda wa pili kutoka kushoto akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wenzie Nandi Mwiyombela wa nne na Bahati Singh aliyesimama nyuma ya Teddy na juma Nature mwenye fulana nyeusi mstari wa mbele pamoja na wasanii mbalimbali jana usiku kwenye tamasha la Fiesta Jipanguse 2010 katika Uwanja wa Mkwakwani mkoani Tanga.
Mashabiki mbalimbali walijitokeza kwenye tamasha hilo kama unavyoona kwenye picha.
Hapa sio kwamba wameamrishwa kunyanyua mikono yao juu hapana, ni burudani ya Fiesta Jipanguse 2010.
Chui wa Serengeti walishiriki kikamilifu katika kunogesha tamasha hilo.
Nao vijana wa kundi maarufu na linalotikisa nchini kwa sasa katika burudani THT lilifanya mambo makubwa jukwaani kutokana na staili mbalimbali za uchezaji wao hivyo kuwafanya mashabiki waliohudhuria kwenye tamasha hilo katika uwanja wa mkwakwani kulipuka kwa shangwe za kujipangusa na Fiesta 2010 kila mara wakati kundi hilo lilipokuwa likicheza jukwaani.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment