WANACHAMA 378 wa chama cha Mapinduzi ( CCM) wamdhamini Kikwete Morogoro!!


Na John Nditi, Morogoro


WANACHAMA 378 wa chama cha Mapinduzi ( CCM) kutoka Wilaya ya Morogoro wamejitokeza kumdhamini, fomu ya mgombea wa kuomba kuteuliwa na CCM katika nafasi ya Urais wa Tanzania kwa miaka mitano , Rais Jakaya Kiwete .

Rais Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa chama hicho Taifa, amechukua fomui kwa ajili ya kugombea urais wa Tanzania kwa tiketi ya CCM kwa kipindi cha miaka mitano ijayo.

Rais Kikwete alichukua rasmi fomu ya kuomba kuteuliwa kuwa mgombea wa nafasi hiyo kubwa Juni 21, mwaka huu Makao Makuu ya Chama hicho Mjini Dodoma.

Wanachama wa chama hicho waliomdhamini ni kutoka Manispaa ya Morogoro na Morogoro Vijijini , ambapo kwa Manispaa Mwanachama wa kwanza kuwekea udhamini wake aliyewahi ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Morogoro , Kanali Mstaafu Izack Mwisongo.

Mbali na Mwenyekiti Mstaafu huyo wa CCM Mkoa wa Morogoro, mwingine alikuwa ni Katibu wa CCM Mstaafu wa Wilaya ya Morogoro Mjini, ambaye pia ni Kapteni mstaafu, Nicholaus Mvanga.

Baadhi ya viongozi wengine wa ngazi za chama hicho waliojitokeza kudhamini fomu za Mgombea wa Urais kupitia CCM, ni Katibu wa CCM Tawi la Mbete, Kata ya Mlimani, Asha Almasi pamoja na Mwenyekiti wa UWT Kata ya Sultan Area, Anuni Jafari.

Kwa upande wa Morogoro vijijini , mgombea huo alipata wadhamini 46 kutoka Matawi ya Mkambarani, Fulwe na Gwata Ujembe, katika Tarafa ya Mikese ambao wengi wao walikuwa ni wazee , vijana na akina mama.

Katibu wa Kamati ya Kusajili wadhamini Kanda ya Mashariki yenye kujumiisha Mikoa ya Morogoro, Pwani, Tanga na Dar es Salaam, Alexandaer Nchimbi alisema wanaccm wenngi walijitokeza kumdhamini mgombea wao Rais Kikwete ,lakini kutokana na muda kuwa mdogo wengi wameshindwa kutimiza kusudio lao.

Nchimbi ambaye ni Mjumbe wa Baraza Kuu wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi ( UVCCM), alisema baada ya kupata wadhamini wengi katika Mkoa wa Morogoro, siku hiyo waliekelea Mkoa wa Tanga na baadaye kuwenda Pwani na kumalizika Jijini Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa Katibu wa Kamati huyo ya Kanda ya Mashariki, idadi hiyo kubwa imaonyesha kuwa wananchi na wanaccm bado wanaimani ya uongozi wa Rais Kikwete na hivyo kujitokeza kumdhamini ili awezekuteuliwa na kuchaguliwa kipindi kingine cha miaka mitano.

Ujumbe wa Kamati hiyo uliambatana na Mwenyekiti wa kitaifa wa uratibu wa zoezi la kupata wadhamini wa fomu ya mgombea huyo zilizogawanywa kuwa Kanda sita na kuhudhuiria katika zoezi lililifanyika Ofisi ya CCM Mkoa wa Morogoro.

Katibu Msaidizi Mkuu wa CCM Mkoa wa Morogoro, Eliud Shemauya, alisema zoezi hilo lilifanyika katika Wilaya mbili za kichama ya Mororogoro mjini na Vijijini ambapo wanachama wengi walijitokeza.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment