Rais Kikwete akutana na Bill Clinton ikulu dar es salaam awaapisha majaji kumi wa Mahakama Kuu!!

Rais Jakaya Mrisho Kikwete leo amewaapisha majaji kumi wa mahakama ya Rufaa katika hafla iliyofanyika ikulu jijini Dar es Salaam.Majaji walioapishwa ni pamoja na John Harold Utumwa,Samwel Victor Karua, Beatrice Rodah Mutungi,Richard Malima Kabela, Grace Kalonge Mwakipesile,Ama-Isario Ataulwa Munisi, Agnes Enos Bukuku, Mwendwa Judith Malecela, Haruna Twaibu Songoro na Dkt Fauz Abdallah Twaib.Katika picha Bibi Mwendwa Judith Malecela akila kiapo mbele ya Rais Jakaya Mrisho Kikwete katika viwanja vya ikulu Dar es Salaam.(picha na Freddy Maro)

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimkaribisha ikulu jijini Dar es Salaam Rais wa mstaafu wa Marekani Bill Clinton leo mchana.Baadaye viongozi hao wawili walifanya mazungumzo.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na katika mazungumzo na Rais Mstaafu wa Marekani Bill Clinton Ikulu jijini Dar es Salaam leo mchana.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment