WANACCM WAENDELEA KUMDHAMINI JAKAYA KIKWETE MJINI DODOMA!!

Jamani napenda kuwapa updates ya kinachoendelea hivi sasa mjini Dodoma. Mambo ni motomoto sasa hivi, na kwa kweli wana CCM wana kila sababu ya kumdhamini Mh. Jakaya Kikwete.

Zoezi linaloendelea sasa hivi ni kwamba wana CCM wa Mkoa wa Dodoma wanatia saini (kudhamini) kwenye fomu za mgombea wa urais kupitia CCM Ndugu Jakaya Mrisho Kikwete. Vijana wa UVCCM ndio wanaoendelea na shughuli hii.
Awali mgombea Urais Mh. Jakaya Kikwete alipita kuwasalimu wana CCM wenzake na kuwashukuru kwa kitendo chao cha kumdhamini ili kuendelea na awamu ya pili ya urais.

Kabla ya hapo, Mgombea pia alipokea michango kutoka vikundi mbalimbali vya wana CCM kumsaidia katika shughuli nzima ya kuzunguka mikoa yote ya Tanzania kuomba udhamini wa kuendelea na uongozi wa CCM ngazi ya juu kabisa.

Wanaccm mbalimbali waliojitokea wakati Jakaya kikwete alipochukua fomu za kugombea urais leo asubuhi.




You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment