Jamani wadau mpira ndiyo umekwisha na timu yetu ya taifa Taifa Stars imefungwa magoli 5-1 kwa kwelii ulikuwa ni mchezo mzuri kwa maana ya wachezaji wetu makocha wa nyumbani wakuu wa TFF pamoja na namshabiki, kuijifunza kutokana na kiwango cha timu ya Brazil ambayo inachukuliwa kuwa ndiyo timu bora na yenye kiwango cha juu cha soka duniani.
Hata hivyo nampongeza mchezaji Jabir Azizi kwa kuifungia Taifa Stars goli zuri kwani Brazil hawajafungwa hata mchezo mmoja wa kirafiki zaidi ya miezi sita iliyopita hivyo Taifa Stars imejiwekea rekodi nzuri dhidi ya Brazil jambo ambalo hata kocha Dunga mwenyewe alikiri na kusema wamepata kipimo kizuri katika mchezo huo mara baada ya kuisha mchezo huo.
Lilikuwa ni jambo jema kwa watu wote pamoja na taasisi za zilizohusika katika kuhakikisha timu ya taifa ya Brazil inakuja hapa nyumbai na inacheza na timu yetu ya taifa ili wachezaji wetu wapate ujuzi na uzoefu kwa kiwango fulani japokuwa ni wazee kwa kiasi, lakini lakini si tatizo hii itakuwa changamoto kwao katika kujiweka sawa na kujifuza mambo mbalimbali yanayohusu mpira, kuwa na nidhamu mchezoni na kujituma.
Nawashukuru Brazil kwa kukubali kuja maana wametutoa tongotongo za soka kwa kiwango fulani japokuwa watanzania kujifunza na kukubali kushindwa ama kujishusha hawapendi na hawataki, lakini ukweli unabaki palepale kwamba timu ya taifa ya Brazil imekuja kutufundisha soka na ni muhimu tukakubali kujifunza kutoka kwao.
Wadau sina mengi ila haya ndiyo niliyokuwa nayo kutoka moyoni mwangu leo na nimeamua kuwafikishia ili nanyi mjumuike katika kuchangia maoni kama mtapenda.
Pia ninawashukuru TFF walioweka kiingilio cha juu sana yaani elfu 30.000 kwa wale watazamaji wa viti vya kijani na bluu, kwani hii imesaididia kuzuia baadhi ya mashabiki wa hali ya chini kutojitokeza kwenda kuangalia mpira huo.
Maana wao mpira hauwafai kwani uwanja ulionekana kuwa mtupu kitu kinachodhihirisha kwamba mashabiki wa kawaida wameshindwa kuingia kwenye mchezo huo kutokana na kiingilio kikubwa kilichowekwa na TFF Hongereni sana TFF.

1 comments:
Kakaaaa, eeh, kaka yangu John, umepasua jipu pasuuuu, pwaaaa!
Naona hii ilikuwa ni mechi ya 'wenyewe' sisi akina 'pangu pakavu tia mchuzi' tumebaki kubabia babia kwingine.
Mi sijalipa hiyo fedha, sijaenda kiwanjani lakini mbayuwayu mie nimeiona mtandaoni 'LIVE' teh!
Brazil 3 Zimbabwe 0
Brazil 5 Tanzania 1
mwe!
Post a Comment