TAHADHARI KWA WATANZANIA WAENDAO NAIROBI!!


Kutoka kwa mdau wa -Nairobi

Napenda kuwatahadharisha watanzania wenzangu ukikutana na mtu usiyemjua akakusalimia na kutaka kukupa mkono please usikubali. Nchini Kenya kuna jamaa anaitwa Philip Onyancha kaua watu 17 wote wanawake na alikuwa amepanga kuua wanawake 100. kawaua thika, naivasha na nairobi amekiri kuua na alikuwa akiua anakunywa damu zao.

Mwalimu wake wa sekondari alimfundisha jinsi ya kuua watu. akikutana na demu akimsalimia dem anamfuata mwenyewe. Akimpa mkono ni kosa yaani utaenda tu. Kama huyo mwanamke ni target yake lazima utamfuata yaani ni kama mbwa akiona nyama. Jana alikuwa anawaonyesha polisi sehemu ambazo ameficha maiti. Kwa kupata habari kamili soma magazeti ya star, the nation, standard, people yote ya nchini Kenya.

Jamaa alikuwa anaeleza jinsi alivyoua bila hata kuogopa kwa raha zake anahojiwa na media na kusema.Siku njema wapendwa na kila laheri katika kusikiliza bajeti yetu leo, kesho ufunguzi wa kombe la dunia yaani hadi raha ila hawa wauaji wanatukosesha raha wanawake. Kwani kama wakikupata wasipokuua lazima watakubaka. Nakutumia na picha ya muuaji ambayo nimeipata kwa hisani ya gazeti la Nation.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment