REDDS MISS ILALA WATEMBELEA KIWANDA CHA TBL LEO!!

Warembo wanaoshiriki katika shindano la kumsaka Redds Miss Ilala 2010 wakiingia kwenye kiwanda cha Kampuni ya bia ya TBL ili kujionea shughuli mbalimbali zinazofanywa kiwandani hapo wakati wa kutengeneza bia zinazozalishwa na kiwanda hicho warembo hao wanatarajia kupanda jukwaani kwenye ukumbi wa Ubungo Plaza juni 26 katika shindano la urembo litakalomtoa malkia wa Ilala mwaka huu, hivi sasa mrembo Sylivia Shally ndiye anayeshikilia Taji hilo baada ya kulichukua mwaka jana.
Hapa wakiangalia jinsi bia inavyojazwa kwenye chupa na kufungwa vizibo kabla ya kupangwa kwenye masanduku tayari kwa kuhifadhiwa ili kuingiza kwenye soko.
Warembo wanaoshiriki katika shindano la Redds Miss Ilala wakielekezwa kitu na bw. Justino Jekela jinsi mtambo wa kuchuja bia unavyofanya kazi wakati walembo hao walipotembelea kiwanda hicho leo mchana.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment