Rais Kikwete atunuku Nishani Dodoma!!

Rais Jakaya Mrisho Kikwete leo ametunuku nishani za madaraja mawili kwa watumishi wa umma waliotumikia kwa muda mrefu na uadilifu.nishani zilizotolewa leo ni pamoja na Nishani ya Utumishi mrefu na Maadili mema daraja la kwanza kwa watumishi wawili na nishani ya utumishi mrefu na Maadili mema daraja la pili iliyotolewa kwa watumishi nane.Pichani Rais Jakaya Kikwete akimtunuku katibu mkuu Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma Bwana George Yambesi Nishani ya Utumishi Mrefu na maadili mema Daraja la Kwanza katika sherehe iliyofanyika katika viwanja vya Nyerere Square mjini Dodoma. (picha na Freddy Maro)

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment