Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wanawake na Watoto Bw. Leon Msimbe akishirikiana na watoto kukata keki wakati wa maadhimisho ya siku ya Mtoto wa Afrika iliyofanyika kwenye Hospitali ya Taifa ya Muhimbili katika jengo la watoto leo, huku ikiambatana na uzinduzi wa Michoro mbalimbali ya picha katika jengo hilo iliyolenga kupendezesha jengo hilo lakini pia kuwavutia watoto kwa picha mbalimbali zenye kufundisha pia.
Michoro hiyo imechorwa kwa Msaada wa kampuni ya East African Elevetor Company ya jijini Dar es salaam ambayo inajihusisha na kufunga na kufanyia matengenezo ya Lifti katika majengo mbalimbali jijini.
Kaimu katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wanawake na Watoto Bw. Leon Msimbe akikata utepe wakati alipokuwa akizindua michoro ya picha mbalimbali zilizochorwa katika Jengo la wodi za watoto katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa msaada wa kampuni ya East African Elevetor Company OTIS katika maadhimisho ya siku ya mtoto wa Afrika iliyofanyika katika hospitali hiyo, kulia ni Mkurugenzi wa OTIS Bw. Justin Lyatuu na kushoto ni Prof. Swai Mkurugenzi wa Huduma za Tiba Muhimbili.
Waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali wakiongea na Elizabert Andrew mama wa mtoto Andrew Issa aliyebebwa na Mpiga picha wa ITV Hughes Dugilo mara baada ya maadhimisho hayo leo kulia ni Zamzam Mwandishi wa Gazeti la Majira na anayefuatia kutoka kulia ni Celina kutoka Gazeti la Uhuru.
Leon Msimbe Kaimu katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wanawake na Watoto akizungumza wakati wa maadhimisho ya Siku ya mtoto wa Afrika iliyofanyika jengo la watoto katika Hospitali ya Muhimbili leo, kulia ni Mkurugenzi wa huduma za Tiba Muhimbili.
Wafanyakazi wa kitengo cha watoto katika Hospitali ya Muhimbili kutoka kulia ni Faraja Mgeni, Judith Kayombo, Dr. Mary Charles na Leokadia Tarimo wakipozi kwa picha wakati wa maadhimisho ya siku ya mtoto wa Afrika yaliyofanyika katika jengo la watoto leo.
0 comments:
Post a Comment