MWENYEKITI WA CHAMA CHA CHADEMA KAWE AJIUZULU!!

Mwenyekiti wa Chama Cha CHADEMA wilaya ya Kawe Bw. Mwenge Mtumwa Jumanne ametangaza kujiuzulu wadhifa huo leo Juni 4-2010 wakati alipoongea na waandishi wa habari kwenye mkutano uliofanyika katika ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo leo jijini Dar es salaam.
Bw. Mwenge amesema ameamua kujiuzulu kwa kuwa chama cha CHADEMA si mali ya wanachama bali ni mali ya kundi dogo la watu ndani ya chama, lakini pia uongozi wa chama mkoa wa Kinondoni haufuati utaratibu uliowekwa wala katiba ya chama hicho katika maamuzi mbalimbali wanayotoa hivyo kuwanyima haki waliowengi.
Amesema anaomba uamuzi wake huo wa kujiuzulu uchukuliwe na uongozi wa juu kama changamoto ya kurekebisha kasoro na mapungufu aliyoyataja katika taarifa yake kwa vyombo vya habari.
Akiwa katika chama cha CHADEMA Bw. Mwenge Mtumwa Jumanne alikuwa na nyadhifa mbalimbali katika chama hicho kabla ya kujiuzulu kwake ambapo alikuwa Mwenyekiti wa wa Kata ya Kunduchi, Mjumbe wa mkutano mkuu Taifa, Mwenyekiti wa Wilaya ya Kawe na mjumbe wa Baraza kuu la CHADEMA.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment