Mvumbuzi wa dawa ya Billyd Fomula Power inayotibu ugonjwa wa Figo Bw. Daniel Paul Kiwauka mazi wa Kiliamnjaro akiongea na waandishi wa habari wakati alipokuwa akilalamikia kitendo cha Mamlaka ya Usimamizi wa Madawa ya binadamu TFDA kupiga marufuku matangazo katika vyombo vya habari mbalimbali jambo ambalo amesema si la haki kwao kwani tayari Wizara ya Afya inawatambua.
Amesema ameshatibu wagonjwa mbalimbali kwa kutumia dawa hiyo na wengi wao wako serikalini na Makampuni mbalimbali na yeye kama mvumbuzi anatambuliwa na Wizara ya Afya na Ustawi wa jamii kwani ameshatunukiwa Cheti na kikombe kama mvumbuzi wa dawa hiyo.
Amesema Nchini kwetu hajathaminiwa laikini akienda nje ya nchi hupokewa kama mfalme kutokana na kukbalikwa kwa tiba yakle hiyo Figo ambayo imesaiduia watu wengi sana nchini na mataifa mengine tofauti.
Kulia katika picha ni mtoto wake anayejulikana kwa jina la Paul Daniel Kiwauka ambaye aliongozana naye katika mkutano huo.
1 comments:
Je Mr Kiwauka anapatikana wapi? Sisi tunaotumia dawa za haemopathy (zisizokuwa na kemikali) tunawahitaji watu kama hawa.
Post a Comment