MTANGAZAJI CYPRIAN MUSIBA ATANGAZA KUMVAA JOHN KAJEGE WA MWIBARA!!


Mwandishi wa habari na Mtangazaji mwandamizi wa Televisheni ya Channel Ten, Cyprian Musiba ambaye ametangaza kugombea Ubunge wa jimbo hilo kupitia CCM, ameonekana kukubalika jimboni Mwibara
Musiba ambaye ni kijana, wiki iliyopita alizuru katika jimbo hilo la Mwibara kwa lengo la kujitambulisha na kutangaza nia yake ya kugombea ubunge wa jimbo hilo, alipokelewa na watu wengi wa rika zote kila alipokuwa akienda kujitambulisha

kwake.
Akizungumza kwa nyakati tofauti na wanachama wa CCM katika vijiji vya vya Karukekere, Chingurubila, Mugara, Mwiruruma, Sikiro, Igundu, Muranda na Buramba, Musiba alisema ameamua kugombea ubunge katika jimbo hilo, ili kuwakomboa wananchi kimaendeleo, kwani jimbo hilo lipo nyuma zaidi kimaendeleo huenda kuliko majimbo yote nchini.

Alisema, tangu nchi ipate Uhuru hadi sasa, wananchi wa Mwibara bado wanapata shida kubwa sana katika suala zima la maendeleo, kwani barabara zilizopo hazipitiki kirahisi, huduma za afya mbovu jambo ambalo inaonekana wananchi kutelekezwa.
Jimbo la Mwibara hivi sasa linawakilishwa na mbunge anayemaliza muda wake, John Kajege (CCM),

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment