MISS ILALA WAKO LAMADA WAKIJIFUA KWA SHINDANO LAO JUNI 26/2010!!

Mwalimu wa warembo Miss Ilala 2010 Slyvia Shally akipozi na warembo katika picha shindano hilo linatarajiwa kufanyika Juni 26 kwenye ukumbi wa Hoteli ya Blue Pear Ubungo jijini Dar es salaam ambapo katika kujizatiti zaidi na mashindano hayo Mwenyekiti wa kamati ya Redds Miss Ilala Miss Jackson Kalikumtima amesema wajiweka sawa na wanamipango madhubuti ili kuhakikisha kwamba burudani zanakuwa bomba siku ya shindano lakini pia shindano lenyewe linakuwa kwenye viwango vya kimataifa kulingana na aina ya wapenzi wa masuala ya urembo .
Vimwana wa Redds Miss Ilala wakiwa katika kivazi cha wadhamini wakuu Vodacom Miss Tanzania wakati wa kupiga picha kwenye kambi yao iliyopo kwenye Hoteli ya Lamada jijini Dar es salaam.
Warembo wanashiriki katika shgindano la Redds Miss Ilala wakiwa katika picha ya pamoja na mwalimu wao Miss Ilala 2010 Slyvia Shaly.
Warembo wanaoshiriki katika shindano la Redds Miss Ilala wakiwa katika vazi la wadhamini wakuu Vodacom Miss Tanzania

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment