DAWA YA MSETO – ALU NI SALAMA, DR.KIGODA!!


Habari Jamal Zuberi na Mwirabi Sise – MAELEZO Dodoma


Serikali imesema, hakuna madhara yoyote ya kiafya yanayoweza kujitokeza kwa binadamu kutokana na utumiaji wa dawa mseto za kutibu ugonjwa wa maralia zinazojulikana kama (ALU).

Hayo yamesemwa leo Bungeni na Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii wakati akijibu swali la mbunge wa Mfenesini Mhe. Mossy Suleiman Mussa alipotaka kujua madhara yanayoweza kutokea kutokana na matumizi ya dawa za malaria aina ya ALU.

Dk. Kigoda amessisitiza kuwa hakuna madhara yoyote ya kiafya kwa binadamu kutokana na dawa hiyo na kusema kwamba Taasisi ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR) umethibitisha ukweli huo.

Mhe. Kigoda ameongeza kuwa, ni muhimu wananchi kutambua kuwa ALU ni moja ya dawa sahihi zilizopitishwa na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kwa ajili ya kutibu ugonjwa wa Maralia.

Amewataka wananchi pamoja na Waheshimiwa wabunge kutokuwa na hofu kuhusiana na matumizi ya dawa hiyo ambayo ni dawa sahihi kwa tiba ya ugonjwa wa maralia.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment