MAMA SALAMA KIKWETE AFUNGUA SEMINA YA MADAKTARI BINGWA DUNIANI!!

Mke wa Raios Mama Salma Kikwete akisoma hotuba yake aliyoitoa katika ufunguzi wa semina ya Madaktari Bingwa wa Magonjwa ya Wanawake na Uzazi duniani figo (FIGO)inayofanyika leo kwenye Hoteli ya Kilimanjaro Kempinski Jijini Dar es salaam Semina hiyo imeandaliwa kwa pamoja na Shirikisho la vyama vya madaktari bingwa hao na (AGOTA) Chama cha Madaktari bingwa wa Magonjwa ya wanawake hapa nchini na lengo la semina hiyo ni kupeana ujuzi na kubadilishana mbinu mbalimbali katika kukabiliana na na magonjwa mbalimbali yanayowapata wanawake na wakati wa kujifungua.

Mdau Gaston na wenzake kutoka PSI hawakuwa nyuma kuonyesha bidhaa yao ya Salama Condom katika mkutano huo kuonyesha kwamba wanajali afya za washiriki wa semina hiyo.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiwasili katika Hoteli ya Kilimanjaro Kempinski leo asubuhi ili kufungua semina ya madaktari bingwa wa magonjwa ya wanawake na Uzazi. wengine katika picha kutoka kulia ni Katibu Mkuu wa AGOTA Fadhiluna Mohamed Ally Dr. Muganyizi mwenyekiti wa AGOTA na Prof. Gamal Serour mwenyekiti wa FIGO chama cha madaktari bingwa wa magonjwa ya wanawake na uzazi cha Dunia.

Washiriki wa semina hiyo wakimsikiliza Mama Salma Kikwete hayupo pichani wakati alipokuwa akitoa hotuba yake.

Madaktari bingwa wa magonjwa ya wanawake na uzazi kutoka nchi mbalimbali Duniani wakiwa katika picha ya pamoja na mgeni rasmi Mama Salma Kikwete.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment