GENEVIVA EMMANUEL NDIYE VODACOM MISS CHANG'OMBE!!


Miss Chang'ombe Geneviva Emmanuel akiwa katika picha ya pamoja na mshindi wa pili Upendo Urasa kulia na mshindi wa tatu Anna Daud mara baada ya washindi kutangazwa katika shindano la Miss Chang'ombe liliofanyika kweny viwanja vya TCC Sigara Jijini Dar es salaam usiku wa kuamkia leo.
Katika shindano hilo lililokuwa la kuvutia kutokana na viwango vya warembo walishiriki kwenye shindano hilo, mashabiki wengi waliinuka na kushangilia kwa nguvu mara baada ya washindi hao kutangazwa huku wakisikika kuwapongeza majaji kwa kazi nzuri kwani walidai kuwa majaji wametenda haki na hawa warembo wamejibu vizuri maswali yao, lakini pia mwaka huu chang'ombe wana wawakilishi wazuri kwenye Miss Temeke hata Miss Vodacom Tanzania Pia.
Katika onyesho hilo burudani ziliporiomoshwa na bendi tya FM Academia na kundi la ngoma za asili la Machozi kutoka jijini Dar es salaam.
Hawa ni Tano bora kuanzia kulia ni Geneviva Emmanuel, Anna Daud, Upendo Urasa, Emaculata Njuu na Jaquiline Benson.
Mh we acha tu! yaani ni burudani kwa kwenda mbele.
wanenguaji wa bendi ya FM Academia wakishambulia jukwaa.
Vazi la ufukweni

Vazi la Ubunifu

Vazi la ubunifu


Vazi la Ubunifu
Warembo wakaingia kwa shoo kabambe
Mmoja wa mashabiki wa Urembo wakishangilia kwa furaha
"Hawa wao walifumwa wakiteta" kulia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Miss Tanzania Prashant Patel na kushoto ni Mkurugenzi wa Miss Tanzania Hashim Lundenga.
(Baba Paroko) Tom Chilala ambaye ni mwandaaji wa Miss Changombe akiwa kwa karibu na mbunge wa jimbo la Temeke Mh. Abbas Mtemvu wakifuatilia kwa makini shindano hilo.
Big Manager Mujibu wa FM Academia akiwa na wanamuziki wa bendi hiyo katikati ni Josse Mara na kulia ni Nyoshi El Sadaat.
Mwandaaji wa Miss Kinondoni Boy George akiwa na Mkurugenzi wa Miss Kinondoni Rahma George wakifuatilia kwa karibu wakati shindano hilo lilipokuwa likiendelea.

Mdau Mac Temba Edwin Tema akiwa na Maiwaifu Wake pembeni.
Mdau Elsi Martin kushoto , akiwa na Jokate Mwegelo katikati na Miss Temeke aliyemaliza muda wake Sia Ndaskoi
Makamu Mwenyekiti wa Kwanza wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini Athuman Nyamlani kulia akiteta jambo na Mkurugenzi wa Gazeti la Jambo Leo Juma Pinto wakati wa shindano la Miss Chang'ombe.

Kikundi cha ngoma za asili cha Mionzi kikitumbuiza wakati wa shindano la Miss Chag'ombe.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment