Watu 104 wafa kwenye ajali ya ndege Lybia!!

Ndege ya shirika la ndege la Afriqiyan kabla ya kuanguka katika uwanja wa ndege mjini Tripoli.

Ndege hiyo baada ya kuanguka

Maafisa nchini Lybia wamesema ndege ya abiria imeanguka katika uwanja wa ndege mjini Tripoli na kuwaua tariban watu 104.Ndege hiyo inayomilikiwa na shirika la ndege la Afriqiyah ilikuwa safarini kutoka mjini Johannesburg, Afrika Kusini.

Maafisa wamesema ilianguka wakati ikjaribu kutua karibu na uwanja huo.Takriban abiria 93 walikuwa ndani ya ndege hiyo aina ya Air Bus 330.

Watu hao wanaaminika kutoka mataifa mbalimbali zikiwemo nchi za Uingereza na Afrika Kusini.Wafanyikazi 11 wa ndege hiyo wameripotiwa kuwa raia wa Lybia.

Ndege hiyo ilitarajiwa kuelekea eneo la Gatwick viungani mji wa London baada ya kusimama kwa muda mjini Tripoli.

Mwandishi wa BBC mjini Tripoli Rana Jawad amesema haijabainika ikiwa ndege hiyo ilikuwa imesha tua wakati ajali hiyo ilipotokea.Walioshudia wamesema hawakuiona ndege hiyo katika uwanja.

Magari ya kuwabebea wagonjwa yanaonekana yakielekea uwanja huo.Shirika la ndege la Afriqiyah lilianzishwa nchini Lybia mwaka wa 2001.


You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment