Washindi wa Kwea pipa wapatikana!!

Nimekutumia press release ya washindi wa tiketi kwenda SA kuangalia mechi ya Kombe la FIFA la Dunia. Mmoja wa washindi hao ni mbunge wa zamani wa jimbo la Kilolo Venance Mwamoto.

Dar es Salaam Mei 5, 2010...Washindi wengine wanane zaidi wa tiketi ikiwa in pamoja na mbunge wa zamani wa Jimbo la Kilolo Mheshimiwa Venance Mwamoto katika promosheni inayoendelea ya Kwea Pipa na Coca-Cola: Shinda tiketi ukasherehekee Kombe la FIFA la Dunia 2010 wametangazwa leo kwenye hafla fupi iliyofanyika Coca-Cola Kwanza, Mikocheni, jijini Dar es Salaam.

Washindi hao watakuwa miongoni mwa washabiki 200 watakaokwenda Afrika Kusini kwa udhamini wa Coca-Cola kutazama mechi ya Kombe la FIFA la Dunia kati ya Brazil na Ureno. Mchezo huo unaotarajiwa kuwa mgumu na wa kusisimua utachezwa Juni 25 kwenye uwanja mpya na wa kisasa wa Moses Mabhida uliopo jijini Durban.

Akitangaza washindi hao Meneja Masoko wa Coca-Cola kwanza Vida Nasari alisema: “Hii ni fursa na zawadi ya pekee kwa wateja wetu ambao wamekuwa wakituunga mkono kwa kutumia bidhaa zetu zinazopendwa na mamilioni ya watu duniani kote”.


Aliwataja washindi wapya wa tiketi kuwa ni Peter Sylvester Ngubi mkazi wa Vingunguti, George Herman Moshi wa Mbezi Beach, Venance M. Mwamoto kutoka Temeke, Gibson Mlaseko mkazi wa Ubungo Kibangu na Kastor Kanyopa wa Kurasini.


Wengine ni Hassan Hamis Nganu wa Yombo Vituka, Gwantwa Kasamala mkazi wa Mbezi Beach na Valentino Mugaya. Nasari aliwataja washindi wa runinga ya kisasa aina ya Sony kuwa ni Zebedayo Kimaro na Denis Methew wote wakazi wa Mbagala nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam.
.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment