FULLSHANGWE IKIWA MISRI INAKULETEA MATUKIO YA MAENDELEO YA KAMBI YA SIMBA!!

Wachezaji wa Simba wakimsikilizaAkizungumza na wachezaji hao mjini hapa juzi Kaimu Balozi wa Tanzania nchini Misri Jestas Nyamanga aliyesimama na viongozi na wa dau mbalimbali wa Simba wakati alipowatembelea katika mazoezi kwenye Hoteli ya Nile Paradise jijini Cairo. FULLSHANGWE itakuwa ikikuletea kila litakalojiri katika katika maadalizi na mchezo kati ya Simba na Haras El Hadood.
Na Mdau Asha Kigundula,Cairo Misri

WACHEZAJI wa Simba wametakiwa kuiondolea Tanzania aibu kwa kuwafunga wapinzani wao katika mchezo wao wa kesho dhidi ya Haras El Hadood utakafanyika mjini Alexandria nchini hapa.

Akizungumza na wachezaji hao mjini hapa juzi Kaimu Balozi wa Tanzania nchini Misri Jestas Nyamanga, alisema kuwa kuwafunga Haras El Hadood kutaijengea nchini heshima.

Nyamanga alisema kuwa ni muhimu mkubwa sana kuweka utaifa mbele kwa kuwa sasa ndiyo timu pekee iliyobaki katika mashindano ya kimataifa kwa Tanzania.

Alisema kuwa Simba ina kila sababu ya kuwatoa wapinzani wao hao kutokana na maandalizi mazuri iliyopata ikiwa ni pamoja na kuweka kambi mjini hapa kwa muda wa siku tano.

Nyamanga alisema kuwa licha ya kuwa wapinzani wao wana mbinu nyingi lakini ana uhakika wachezaji hao wakiamua wana uwezo mkubwa wa kuwang’oa wapin zani wao.

Naye Afisa wa Ubalozi Ibrisa Juma alisema kuwa kutokana na kauli za wamisri kwa timu za Tanzania itakuwa jambo kubwa na nzuri kwa timu ya Simba kuwaondoa wapinzani wao hao.

Juma alisema kila mara wamekuwa wakizomewa kwa kuwaambiwa timu za Tanzania haziwezi kufanya lolote katika mashindano yoyote nchini hapa.

“Tuna kila sababu ya kujivunia kwa kuwaondoa wapinzani wetu katika manshindano haya wanatudharau sana…endapo tutawaondoa nasiu watatuheshimu”alisema Juma.



wachezaji wa simba wakimsikiliza kaimu Balozi wa Tanzania nchini Misri.
Mdau Asha Kigundula wa gazeti la Jambo Leo aliyekaa kutoka kushoto akiwa na mdau wa Simba, Mulamu Ghambi, na Inocent Njovu wakifuatilia mazoezi ya timu ya Simba yanayofanyika katika hoteli ya Nile Paradise ambako timu hiyo imepiga kambi.
Kutoka klia ni Meneja wa timu Inocent Njovu Mulamu Ghambi kutoka Friends of Simba na mwisho kushoto ni Edo Kumwembe na mdau mwingine jina halikupatikana wakiangalia mazoezi ya Timu ya Simba.
Balozi Jestas Nyamanga akiongea na baadhi ya viongozi wa Simba waliopo nchini Misri katika Hotli ya Nile Paradise Hotel jijini Cairo ikiwa ni maandalizi ya mchezo huo.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment