Mwanamuziki Siza Azizi kushoto na Mwanamuziki Banana Zoro ambaye ni kiongozi wa bendi ya B. Band wakionyesha uwezo wao jukwaani wakati walipofanya onesho na bendi yao kwenye klabu ya Thai Vollage Masaki jijini Dar es salaam usiku wa kuamkia leo.
Katika onesho hilo pia warembo wanaoshiriki katika shindano la RBP Miss Dar Inter College walitembelea kwenye klabu hiyo kwa ajili ya kutambulishwa zaidi kwa mashabiki wa urembo kabla ya shindano lao linalofanyika wiki ijayo mei 27 kwenye klabu ya Billicanas.
Katika shindano hilo pia kutakuwa na burudani kutoka kwa vijana wawili Barnaba na Amini kutoka THT.
Mwanamuziki Banana Zoro na Reah Muddy wakifanya vitu vyao jukwaani wakati wa onesho lao lililofanyika jana kwenye klabu ya Thai Village usiku wa kuamkia leo.
Hapa ni Full mzuka kama unavyowaona warembo wakijimwaga stejini na kujipa raha zao.
Warembo wanaoshiriki shindano la RBP Miss Dar Inter College wakijimwaga kwa raha zao kwenye klabu ya Thai Village usiku wa kuamkia leo ambako mwanamuziki Banana Zoro pamoja na bendi yake ya B. Band walikuwa wakifanya onesho lao.
Wadau wanaoandaa shindano la RBP Dar Inter College wakawa katika picha ya pamoja wakati walipotembelea klabu ya Thai Village pamoja na warembo wanaoshiriki shindano la Miss Dar Inter College.
Mtu mzima Ally Zoro katikati akiwa na vijana wake Banana Zoro kulia na Siza Azizi wakati wa onyesho la bendi ya vijana wake hao lililofanyika kwenye klabu ya Thai Village Masaki jana.
0 comments:
Post a Comment