Katibu mkuu Wizara ya Habari Utamaduni na Michezo Bw. Sethi Kamuhanda akizungumza na wafanyakazi na viongozi wa Idara ya Michezo kutoka Wizara ya Habari, Utamaduni na Michezo leo jijini Tanga. Pamoja na mambo mengine amezungumzia azma ya serikali katika kuboresha sekta ya michezo kwa kuongeza wataalam wa michezo nchini,ushirikishaji wa sekta binafsi na uimarishaji wa Michezo mashuleni.
Na. Aron Msigwa – MAELEZO.
Tanga, 26/5/2010.
Changamoto imetolewa kwa Wafanyakazi nchini kufanya kazi kwa bidii ili kukuza pato la taifa.
Changamoto hiyo ilitolewa jana jijini Tanga na Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari na Utamaduni Bw. Sethi Kamuhanda wakati akihitimisha mkutano wa sita wa baraza la wafanyakazi wa Wizara ya Habari, Utamaduni na Michezo.
Alisema wafanyakazi wanao wajibu na jukumu kubwa la kutumia rasilimali na fursa walizonazo kuleta ufanisi mahali pa kazi sanjari na kuhakikisha kuwa michango ya huduma wanazozitoa zinawafikia walengwa husika katika jamii.
Alifafanua kuwa serikali kwa kutambua mchango wa wafanyakazi itaendelea kuboresha huduma mbalimbali za kiofisi zikiwemo nyenzo mbalimbali za kufanyia kufanyia kazi zikiwemo huduma za usafiri ili kuweka mazingira mahali pa kazi .
Aliongeza kuwa serikali kupitia sekta mbalimbali itaendelea kutoa fursa zaidi kwa wafanyakazi kupata nafasi za masomo kwa lengo la kuinua viwango vya elimu kwa lengo la kuwajengea uwezo wa kufanya kazi kwa ufanisi na kuendana na mabadiliko ya sayansi na teknolojia nchini.
Awali akizungumza kuhusu mkutano Baraza la wafanyakazi Bw. Sethi Kamuhanda alisema mkutano huo umetoa changamoto na kuamsha ari kwa wafanyakazi kwa sababu umezishirikisha ngazi zote za uongozi huku akitoa wito kwa wafanyakazi kutekeleza yale waliyokubaliana katika mkutano huo.
Aidha Bw. Sethi Kamuhanda aliwapongeza baadhi ya wafanyakazi wa Wizara ya Habari, Utamaduni na Michezo waliopata bahati ya kuchaguliwa kuwa wafanyakazi bora na kusema kuwa wao ni mfano wa kuigwa.
“Kuchaguliwa kwenu kusiwafanye mbweteke bali kuwe kichocheo na kuwafanye kuongeza bidiikatika utendaji wa kazi za kila siku ndani ya wizara, napenda kuwasihi wafanyakazi wengine waogeze bidii ili tushirikiane katika kuleta tija na ufanisi mahali pa kazi” alisema.

0 comments:
Post a Comment