VODACOM MISS IFM 2010 KUFANYIKA OYSTERBAY POLICE MESS!!

Makamu mwenyekiti wa Miss IFM Razaro Lutobeka akizungumza na waandishi wa habari kwenye mkutano uliofanyika leo kwenye ukumbi wa Breakpoint Posta wakati alipotangaza zawadi na kuwaonyesha warembo watakaoshiriki kwenye shindano hilo linalotarajiwa kufanyika kwenye bwalo la maafisa wa Polisi Oysterbay Mei 14 mwaka huu jijini Dar es salaam.
Razaro amesema warembo watakaoshiriki katika shindano hilo ni 10 na amewataja kuwa ni Flora Martin,Happy Steven, Anita Petro,Grolia Moshi,Mary IsaackPendo Sam,Judith Osima,Esther Emmanuel,Elitruda Msoka, Surayna Mwarwilo, Christina Marcusna Diana Mosha.
Amesema mwaka huu wameboresha zaidi zawadi za washindi baada ya kukaa na kuamua kupanga mikakati mipya zaidi ya ile ya mwaka jana, amesema mshindi wa kwanza atajipatia shilingi laki 700,000 na vocha ya kufanya manunuzi kwenye duka la Mwasu Fashion yenye thamani ya shilingi laki 300,000.
Mshindi wa pili atapata shilingi 500,000, mshindio wa tatu atapata shilingi300,000, mshindi wa nne atapata shilingi laki 200,000 na mshindi wa tatu atapata shilingi laki 200,000 washiriki wengine watapata kifuta jasho cha shilingi 100,000.
Viingilio katika onyesho hilo vitakuwa kati ya shilingi elfu 8.000 ukinunua tiketi mapema lakini siku ya onesho tiketi zitauzwa shilingi elfu 10,000, onesho hilo linatarajiwa kupambwa na burudani kutoka kwa wasanii Chid Benz na Duly Sykes wakishirikiana na wasanii chipukzi kutoka chuo cha IFM.
Wengine waliopo katika picha kutoka kulia ni Sam Mshana kutoka Mwasu Fashion, Ibrahim Kaude Ofisa katika kitengo cha Udhamini kutoka kampuni ya Vodacom Tanzania ambao ndiyo wadhamini wakuu wa shindano hilo na Peter Sarungi mwenyekiti wa kamati ya Miss IFM.
Warembo wanaoshiriki katika shindano hilo wakiwa katika picha ya pamoja leo baada ya mkutano na wanahabari.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment