Mwenyekiti wa kampuni ya bia ya Serengeti Breweriers Jaji Mark Bomani kulia pamoja na Mkurugenzi wa Masoko wa kampuni hiyo Shantanu Chitgopkar wakionyesha mfano wa bia ya Uhuru Peak Lager jana mara baada ya kuzinduliwa rasmi jijini Dar es salaam kwenye Hoteli ya Movenpick, bia hiyo kwa sasa inapatikana kwenye baa mbalimbali na ina kilevi asilimia 5.8 haya kazi kwenu watumiaji wa kilaji endeleeni kujimwaga na Uhuru Peak Lager.
Kundi la Wanne Star likitumbuiza kwenye uzinduzi huo.
Deo Mwanambilimbi pamoja na bendi ya Kalunde wakitumbuiza katika uzinduzi huo.
Deo Mwanambilimbi pamoja na bendi ya Kalunde wakitumbuiza katika uzinduzi huo.
Mwenyekiti wa Kampuni ya bia ya Serengeti Jaji Mark Bomani akizungumza mbele ya wageni waalikwa wakati wa uzinduzi wa bia ya Uhuru Peak Lager inayotengenezwa na kampuni hiyo uliofanyika kwenye hoteli ya Movenpick jana kulia ni Meneja mkuu wa Uhusiano na Mawasiliano Teddy Mapunda
Teddy Mapunda kushoto na Nandi Mwiyombela wakijaribu kuweka mambo sawa ili kuwaonyesha wageni waalikwa Tangazo la kinyaji cha Uhuru Peak Lager.
Wadau mbalimbali wakikata kinywaji cha Uhuru Peak Lager katika uzinduzi rasmi wa kilaji hicho uliofaqnyika jana kwenye Hoteli ya Movenpick.
Kocha wa timu ya taifa Taifa Stars Marcio Maximo akiwa na maiwaifu wake.
Brand Meneja wa SBL Nandi Mwiyombela kulia akiwa na mdau Said Bonge wa Clouds.
Mzee Leornard Lupilya kulia ambaye alipanda na bia ya Uhuru katika kilele cha mlima Kilimanjaro akiwa na Mwenyekiti wa chama cha Mapinduzi mkoa wa Dar es salaam Mzee Mikidad Mahmoud.
Meneja Mkuu wa Uhusiano na Mawasiliano wa SBL Teddy Mapunda kushoto akiwa na wadau waliohudhuria katika uzinduzi huo uliofanyika kwenye hoteli ya Movenpick jana jioni.
0 comments:
Post a Comment