Ubalozi wa Marekani nchini Tanzania
Tamko kwa Vyombo vya Habari
Mei 20, 2010
Siku ya Jumapili, tarehe 16 Mei, mnamo saa 2.30 usiku, mvulana mwenye umri wa miaka 15 alikimbia na kumpita mlinzi aliyekuwa mbele ya Ubalozi wa Marekani, akawasha moto kwenye chupa iliyokuwa na mafuta ya taa na kisha kuirusha chini ya moja ya malori mawili ya kubebea maji yaliyokuwa yameegeshwa nje ya ukuta wa Ubalozi.

Chupa hiyo ilivunjika lakini haikuweza kulipua moto. Walinzi wa Kampuni ya KK wanaolinda ubalozini hapo walimkamata mara moja kijana huyo kabla hajaweza kurusha chupa ya pili. Hakukuwa na mtu yeyote aliyejeruhiwa wala mali yoyote iliyoharibiwa katika tukio hilo. Askari wa Jeshi la Polisi la Tanzania aliwasili sehemu ya tukio sekunde chache baadaye na kumkamata mtuhumiwa. Jeshi la Polisi linaendelea na uchunguzi.
Baadhi ya maelezo yanayotolewa kuhusu tukio hili si sahihi, yamekuzwa na kutiwa chumvi mno na yasiyo ya kweli, yakidai kuwa mvulana huyo aliingia ndani ya ubalozi. Hii si kweli. Hakukuwa na mtu yeyote aliyeweza kuingia ndani ya Ubalozi wa Marekani.
Taratibu zetu za kiusalama za kuzuia wahalifu kuingia ubalozini zilidhihirisha ufanisi wake hapo Mei 16. Walinzi wa kampuni ya KK na Polisi wa Tanzania walishughulikia suala hili kwa weledi mkubwa. Tunawashukuru sana.
0 comments:
Post a Comment