Rais Kikwete aongoza harambaee kuichangia CCm mkoa wa Kilimanjaro!!

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimtunuku cheti maalumu Katibu Mkuu Kiongozi Philemon Luhanjo kwa kutambua mchango wake katika kufanikisha kwa ufanisi mkubwa kufanyika kwa mkutano wa World Economic Forum uliofanyika jijini Dar es Salaam wiki iliyopita.Katika hafla hiyo wadau wengine wakiwamo mashirika mbalimbali,kampuni na watu binafsi nao walitunukiwa vyeti kwa kufanikisha mkutano huo wa kimataifa.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimkabidhi sanamu ya Twiga Waziri Kiongozi wa Serkali ya Mapinduzi ya Zanzibar Shamsi Vuai Nahodha wakati wa hafla ya uchangiaji fedha kwaajili ya Uchaguzi Mkuu CCM mkoa wa Kilimanjaro iliyofanyika jana jioni katika hoteli ya Golden Tulip jijini Dar es salaam.Sanamu hiyo iliyonunuliwa katika mnada huo na wafanyabishara vijana katika soko la Kariakoo iliuzwa kwa shilingi laki saba na vijana hao kuamua kumpatia zawadi Waziri kiongozi.Katika Harambee hiyo jumla ya shilingi Milioni mia mbili( 200m/-) zilipatikana ikiwa ni fesha taslimu na ahadi.Waziri Kiongozi Shamsi Vuai nahodha alichangia fedha taslimu shilingi milioni moja.
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Kilimanjaro Mama Vicky Nsilo Swai akimzawadia Rais Kikwete Ramani ya Afrika yenye kuwaonyesha wanyama watano wakubwa(the big five) Simba,Tembo,Faru, Nyati na Chui muda mfupi baada ya kumalizika hafla ya kuchangia fedha kwaajili ya Uchaguzi Mkuu CCM mkoa wa Kilimanjaro jana jioni katika hoteli ya Golden Tulip jijii Dar es salaam.Katika hafla hiyo Zaidi ya shilingi milioni mia mbili zilipatikana ikiwemi ahadi na fedha taslimu(picha na Freddy Maro)
-Mwenyekiti wa CCM Taifa Rais Jakaya Mrisho Kikwete akifungua harambee ya kuchangia fedha uchaguzi mkuu CCM mkoa wa Kilimanjaro iliyofanyika katika hoteli ya Golden Tulip jijini Dar es Salaam jana jioni.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment