Nyoka wawa kivutio maadhimisho wiki ya utamaduni.

Wakina mama kutoka mkoa wa Singida na Dodoma wakishindana kusaga karanga kwa kutumia njia ya asili wakati wa maadhimisho ya siku ya utamaduni inayoendelea katika viwanja vya Mandela Mkoani Singida, Hata hivyo Bi.Ukende Zefania (kushoto) kutoka wilaya ya Ilamba aliibuka mshindi.
Picha na Aron Msigwa – MAELEZO

Mzee Juma Mkonko (kushoto) kutoka katika kijiji cha Mwenge,wilaya ya Sikonge mkoa wa Tabora akicheza na Nyoka wakati kundi lake likicheza ngoma aina ya Uyeye ambayo huchezwa na kabila la Wanyamwezi leo wakati wa maadhimisho ya siku ya utamaduni inayoendelea katika viwanja vya Mandela Mkoani Singida.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment